Bomba la Mafuta Uganda-Tanzania Kuzalisha Ajira Elfu 10

Bomba la Mafuta Uganda-Tanzania Kuzalisha Ajira Elfu 10

Na. Georgina Misama-MAELEZO Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan na Rais wa Jamhuri ya Uganda, Yoweri Museveni wameshuhudia zoezi la utiaji saini  ya mradi wa bomba la mafuta ghafi Afrika Mashariki, leo Ikulu Jijini Dar es salaam. Akizungumza katika hafla ya utiaji saini makubaliano ya ujenzi wa mradi huo, Rais Samia

Na. Georgina Misama-MAELEZO

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan na Rais wa Jamhuri ya Uganda, Yoweri Museveni wameshuhudia zoezi la utiaji saini  ya mradi wa bomba la mafuta ghafi Afrika Mashariki, leo Ikulu Jijini Dar es salaam.

Akizungumza katika hafla ya utiaji saini makubaliano ya ujenzi wa mradi huo, Rais Samia Suluhu Hassan amebainisha faida ambazo watanzania watapata kutokana na mradi huo, kubwa ikiwa ni fursa za ajira kwa nafasi mbalimbali hasa kwa mikoa 8 ambayo inapitiwa na ujenzi wa mradi huu.

“Mradi wa ujenzi wa bomba la mafuta utatufanyia jambo kubwa wantanzania ambalo ni fursa za ajira hasa kwa mikoa nane ambayo imepitiwa na mradi huo. Tunatarajia kupata fursa za ajira takribani elf 10 kwa kipindi cha ujenzi kwani asilimia 80 ya ujenzi wa bomba hilo utafanyika hapa Tanzania na asilimia 20 utafanyika Uganda.” Amesema, Rais Samia.

Rais Samia pia amesema utekelezaji wa mradi huu utazidi kuimarisha uhusiano mzuri na wa kihistoria uliopo kati ya Tanzania na Uganda kitu ambacho kitapanua uwanda wa mwingiliano  baina ya nchi hizi mbili.

Aidha, Rais Samia ameyashukuru makampuni yaliyoshiriki katika mchakato huu yakijumuisha Total Afrika, Kampuni ya Taifa ya Mafuta ya Uganda, Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) na Shirika la Taifa la Mafuta la China (CNOOC).

Kwa upande wake Rais wa Jamuhuri ya Uganda, Yoweri Kaguta Museveni amesema kwamba tukio hili la kushuhudia kutiwa saini kwa mkataba wa Nchi Hodhi za mradi wa ujenzi wa bomba la mafuta  ni jambo la kihistoria  na amempongeza  Rais, Samia pamoja na wadau wengine kwa kuhakikisha wanafanikisha.

“Nafikiri Hayati Mwalimu Nyerere pia atakuwa amefurahia kukamilika kwa jambo hili huko aliko kwani tulikuwa tukilijadili sana wakati wake” amesema Rais, Museveni.

Akizungumzia faida kwa nchi zote mbili, Rais Museveni anasema kwamba mradi wa bomba la mafuta ni chachu ya kukuza sekta nyingine za maendeleo kama kilimo, viwanda, teknolojia pamoja na miundombinu kwa kutumia fedha zitakazopatikana kwenye mradi huo.

“Tutatumia rasilimali hizi zenye ukomo (mafuta) kuwekeza kwenye maeneo mengine yasio na mwisho kama kilimo, viwanda na miundombinu ili siku moja mafuta yakiisha tuwe tumefikia hatua nyingine ya maendeleo” Anasema Rais Museveni.

Rais Meseveni aliongeza kuwa ujenzi wa mradi wa bomba la mafuta kutoka Hoima-Uganda hadi Chongoleani Tanga- Tanzania unaweza pia kutumika kusafirishia gesi kwa siku zijazo, ili Uganda iweze kutumia gesi iliyopo Tanzania kwa maendeleo ya viwanda kwani Uganda haina nishati hiyo.

Naye, Waziri mwenye dhamana ya Nishati nchini, Dkt. Medard Kalemani amebainisha faida za Tanzania kuwa nchi hodhi za mradi huo ikiwa ni pamoja na kushiriki katika umiliki wa bomba hilo kwa asilimia 15, huku kukamilika kwa ujenzi wa bomba hilo,  utaifanya Tanzania kupata asilimia 60 ya mapato yote yatokanayo na ujenzi huo.

Waziri Kalemani pia amesema kwamba Tanzania itakusanya kodi kutoka kwenye mradi huo kwa miaka 25, ambapo inatarajiwa kupata kiasi cha dola za Kimarekani milioni 290. Wakati huo huo kampuni zote zitakazotumika kwenye ujenzi wa mradi huo zinatarajiwa kulipa kodi ya kiasi cha dola za Kimarekani  milioni 59 na bandari dola za Kimarekani milioni 73 hii itapelekea chumi kwa fedha za kigeni kuongezeka kwa asilimia 55.

Hatua hii ya kusaini Mkataba wa mradi wa bomba la mafuta kutoka Ohima Uganda mpaka Chongoliani Tanga Tanzania ni mwendelezo wa taratibu za mikataba ya kusheria ambapo mkataba wa kwanza ulisaini tarehe 25 Mei, 2017 nchini Uganda. Mikoa 8 ya Tanzania itapitiwa na mradi huo, ikijumuisha Kagera, Geita, Tabora na Shinyanga. Mikoa mingine ni pamoja na Dodoma, Singida, Manyara na Tanga.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »