CHONGOLO AWATAKA WANACCM MOROGORO KUEPUKA MAJUNGU

CHONGOLO AWATAKA WANACCM MOROGORO KUEPUKA MAJUNGU

WANACHAMA wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) mkoa wa Morogoro wametakiwa kuacha majungu na badala yake wametakiwa kufanya kazi zenye kuleta maendeleo kwa mawanchi kwa kutekeleza ilini cha chama chao.   Wito huo ulitolewa jana na Katibu Mkuu wa chama hicho taifa Daniel Chongolo mkoani hapa akiambatana na Naibu Katibu Mkuu Bara Christina Mdeme pamoja na Katibu wa Itikadi

WANACHAMA wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) mkoa wa Morogoro wametakiwa kuacha majungu na badala yake wametakiwa kufanya kazi zenye kuleta maendeleo kwa mawanchi kwa kutekeleza ilini cha chama chao.  

Wito huo ulitolewa jana na Katibu Mkuu wa chama hicho taifa Daniel Chongolo mkoani hapa akiambatana na Naibu Katibu Mkuu Bara Christina Mdeme pamoja na Katibu wa Itikadi na Uwenezi Shaka Hamidu Shaka walipokuja kujitambulisha.

Chongolo alisema wapo baadhi ya wanachama wamekuwa wakitumia muda mwingi kufanya majungu badala ya kufanya kazi ya kutekeleza ilani ya chama ambapo aliwataka kuachana na tabia hiyo na badala yake wafanye kazi vizuri.

“Lengo la chama chetu ni kutekeleza ilani ya chama chetu kwa manufaa ya wananchi wote katika suala zima la kuleta maendeleo hivyo hatamvumilia mtu atakayeendekeza majungu na fitina ndani ya chama chetu”alisema Chongolo.

Alisema wananchi wanakabiliwa na changamoto nyingi hivyo kwa kuwa CCM imepewa ridhaa ya kuongoza taifa hili kila mwanaccm anataliwa kuwa mstari wa mbele kuhakikicha changamoto zote zilizopo katika jamii zinanatuliwa haraka.

Katibu Mkuu huyo alisema mkoa wa Morogoro umejaliwa kuwa na rutuba inayofaa kwa kilimo cha mazao mbalimbali ambapo alitaka ardhi itumike vizuri kwa uzalishaji wa mazao huo ikiwa ni pamoja na kuepuka migogoro ya ardhi.

Aidha alisema kuwa changamoto ya barabara ya Mikumi IFakara hadi Malinyi amaechukuwa na kuahidi kuanza kuifanyia kazi kuanzisa sasa ambapo pia alisema vijiji vyote ambavyo havina huduma ya umeme ni lazima vipate huduma hiyo.

“Viongozi wa chama tunatakiwa kisimamia miradi yote ya maendeleo na kama kutakuwa na dosari ya aina yoyote tunatakiwa kushauri nini cha kufanya na siyo tu kunyoosheana vidole kwani lengo letu ni kuisimamia serikali”alisema Chongolo.

Naye Naibu Katibu Mkuu wa CCM Tanzania Bara Christina Mdeme ambaye pia ni mlezi wa chama mkoa huo aliwataka wanachama kumuunga mkono kwa dhati rais Samia Suluhu Hassan na pia alisema ni wajibu wa kila kiongizi wa chama kututatua kero kwa jamii.

“Kila nipatokuwa nikiingia kwenye ofisi za viongozi wa chama hiki cha kwanza kabisa nitakachotaka kukifahamu ni namna ya kiongozi huyo alivyoweza kutatua, nitakagua mafaili ya utatuzi wa changamoto hiyo tofauti na hapo hatutaelewana”alisema Christina.

Aidha alikemea ulasimu kwa wawekezaji na kutaka serikali ihakikishe inaweka mazingira mazuri ya wawekezaji katika mkoa huo ambao wataleta tija katika suala zima la maendeleo kwa wananchi wote wa Morogoro na taifa zima kwa ujumla.

Naibu Katibu Mkuu huyo alimpongeza Doroth John Mwasansu kwa kuchahuliwa kuwa Mwenyekiti wa Chama hilo ngazi ya mkoa na kuwa mwanamke wa kwanza kushika wadhifa huo ambapo aliwataka wanachama wa Morogoro kumpa ushirikiano.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Morogoro Doroth John Mwasansu aliwapongeza viongozi hao kwa kuteuliwa na rais Samia Suluhu Hassan kuwa viongozi wa taifa wa chama chao na kuahidi kuwapa ushirikiano.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »