TIC kuimarisha mifumo ya uwekezaji Nchini

TIC kuimarisha mifumo ya uwekezaji Nchini

Na Beatrice Sanga, MAELEZO. Kituo cha Uwekezaji Tanzania-TIC kimeanza kufanya maboresho ya huduma za uwekezaji kwa kuunganisha mifumo ya kielektroniki kwataasisi na idara 11 za Serikali zinazotoa huduma za mfumo wa mahala pamoja lengo likiwa ni kurahisisha utoaji wa vibali na leseni zauwekezaji kwa kuunganisha mifumo hiyo ili kuwa na dirisha moja la uwekezaji nchini

Na Beatrice Sanga, MAELEZO.

Kituo cha Uwekezaji Tanzania-TIC kimeanza kufanya maboresho ya huduma za uwekezaji kwa kuunganisha mifumo ya kielektroniki kwa
taasisi na idara 11 za Serikali zinazotoa huduma za mfumo wa mahala pamoja lengo likiwa ni kurahisisha utoaji wa vibali na leseni za
uwekezaji kwa kuunganisha mifumo hiyo ili kuwa na dirisha moja la uwekezaji nchini


Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) Dkt. Maduhu Kazi amesema maboresho hayo yatasaidia kuongeza ufanisi
katika kutoa huduma za wawekezaji na kuimarisha utendaji kazi wa kituo hicho ikiwa ni agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mhe. Samia Suluhu Hassan alilolitoa Aprili, 2021 wakati akiwaapisha makatibu wakuu wa Wizara.


Dkt Maduhu amefanya kikao cha pamoja na wakuu wa Taasisi na Idara za Serikali 11 zinazotoa huduma kwenye Kituo cha huduma kwa
wawekezaji cha mahali pamoja (One Stop Facilitaion Centre) na kubainisha kuwa mchakato wa maboresho hayo unaendelea kufanyiwa
kazi.
“Kama mnavyofahamu, Mheshimiwa Rais alitoa maelekezo ya namna ya kuboresha huduma za uwekezaji, kikao hiki ni muendelezo wa
utekelezaji wa majukumu hayo, tulishaanza kuyafanyia kazi, na sasa tunaendelea, lengo ni kutoa huduma bora zaidi za uwekezaji”
amesema Dkt. Maduhu.


Katika kikao hicho, Dkt. Maduhu amepokea taarifa ya hatua ambazo zimechukuliwa kwa kila Taasisi na Idara husika zikiwepo kila taasisi
kufungua mfumo wa kielektroniki kwa ajili ya utoaji vibali na leseni mbalimbali, kuunganisha mifumo hiyo ili kuwa na dirisha moja la
huduma kwa wawekezaji nchini na taasisi husika kukamilisha hatua zote ikiwepo kuchambua na kutoa maamuzi kwa maombi husika ya
wawekezaji.


Maboresho haya yanaelezwa kuwa yatawawezesha wawekezaji wanaowekeza nchini kupata huduma kwa muda mfupi na kwa kutumia
gharama ndogo.

Baadhi ya Taasisi zilizoshiriki katika kikao hicho ni pamoja na Uhamiaji, Wakala wa Usalama na Afya Mahala pa Kazi (OSHA), Mamlaka ya
Chakula na Dawa (TMDA), Mamlaka ya Mapato Tanzani (TRA), Baraza la Taifa la Usimamizi wa Mazingira  (NEMC), Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Shirika la Viwango Tanzania (TBS) naOfisi ya Waziri Mkuu
(Kazi).

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »