MKURABITA Yawezesha Wafugaji 58 Mbarali Kijikwamua Kiuchumi

MKURABITA  Yawezesha Wafugaji 58  Mbarali Kijikwamua Kiuchumi

Na Mwandishi wetu- Mbarali Wafugaji 58 wa jamii ya Wamasai   wilayani  Mbarali mkoani Mbeya wamenufaika na mafunzo ya kuwajengea uwezo wa kujikwamua kiuchumi yaliyofanyika katika kijiji cha Mogelo, wilayani humo mwishoni mwa wiki ili kuwawezesha kuendana na dhamira ya Serikali ya Awamu  ya Sita inayolenga kuendelea kuleta mageuzi  ya kiuchumi  kwa wananchi wote.   Mafunzo

Meneja Urasimishaji Ardhi Vijijini kutoka MKURABITA, Bw. Antony Temu akieleza umuhimu wa jamii  ya wafugaji  wilayani Mbarali (hawapo pichani) kutumia hatimiliki za kimila za kumiliki ardhi kujiletea maendeleo ikiwemo kukopa katika mabenki, hayo yamejiri mwishoni mwa wiki wakati wa mafunzo kwa jamii hiyo.
Sehemu ya jamii ya wafugaji wilayani Mbarali  walionufaika na mafunzo ya kuwajengea uwezo ili waweze kutumia hatimiliki za kimila za kumiliki ardhi kujikwamua kiuchumi wakifuatilia mafunzo hayo mwishoni mwa wiki katika kijiji cha Mogelo wilayani humo.
Meneja Urasimishaji Ardhi Vijijini wa Mpango wa Kurasimisha Risilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania (MKURABITA), Anthony Temu akimuelekeza jambo kwenye simu janja mmoja wa vijana wa jamii ya wafugaji,  Mussa Letema wakati wa zoezi la kukusanya taarifa za dodoso kupitia mfumo wa Kobo wakati wa mafunzo ya kuwawezesha kiuchumi watu wa jamii ya wafugaji kwa kutumia hatimiliki za kimila za kumiliki ardhi kuweka kama dhamana kukopa fedha benki za kusaidia kuboresha mfumo wa ufugaji ikiwa ni  pamoja na kuanzisha miradi mingine ili kuinua kipato chao.
Afisa Ushirika wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali, Grace Samwel akielezea sheria na taratibu za kuanzisha ushirika wa Jamii ya wafugaji na faida lukuki watakazopata.
Afisa Ushirika wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali, Grace Samweli (wakwanza kulia) akiingiza kwenye simu janja taarifa za dodoso kwa kutumia mfumo rahisi wa ukusanyaji wa taarifa wa Kobo.
Afisa Mahusiano  NMB  wilaya ya Mbarali, Jones Mugyabuso akielezea umuhimu wa jamii ya wafugaji kujiunga na benki hiyo ili wapate mikopo ya kuwawezesha kutekeleza shughuli za uzalishaji ikiwemo kilimo na  kunenepesha mifugo hivyo kuweza kujikwamua kiuchumi.

Na Mwandishi wetu- Mbarali

Wafugaji 58 wa jamii ya Wamasai   wilayani  Mbarali mkoani Mbeya wamenufaika na mafunzo ya kuwajengea uwezo wa kujikwamua kiuchumi yaliyofanyika katika kijiji cha Mogelo, wilayani humo mwishoni mwa wiki ili kuwawezesha kuendana na dhamira ya Serikali ya Awamu  ya Sita inayolenga kuendelea kuleta mageuzi  ya kiuchumi  kwa wananchi wote.  

Mafunzo hayo yaliyoratibiwa na Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania (MKURABITA) yamejikita katika kuwezesha jamii hiyo ya wafugaji  kutumia hatimiliki za kimila za kumiliki ardhi kukopa fedha katika taasisi za fedha kama benki ili kukuza shughuli za uzalishaji na kujiletea maendeleo ya kiuchumi na kijamii.

Awali akieleza kuhusu mafunzo hayo, Meneja Urasimishaji Ardhi  Vijijini kutoka MKURABITA, Bw. Antony Temu alisisitiza kuwa” Lengo kuu la mafunzo haya ni kuwawezesha wanufaika wote wa mafunzo kutumia hatimilki zao kujikwamua kiuchumi kupitia mikopo inayotolewa na taasisi za fedha ili dhamira ya Serikali   kumuwezesha kila mwananchi iweze kutimia kwa wakati.”  

Aidha, Bw. Temu alieleza kuwa  mada zilizowasilishwa katika mafunzo hayo ni pamoja na; faida za kujiunga na ushirika, mbinu za ufugaji bora, kanuni za kilimo bora cha mazao mbalimbali, utunzaji  bora  wa kumbukumbu na usimamizi bora wa rasilimali zinazoizunguka jamii hiyo.

Wawezeshaji katika mafunzo hayo walikuwa wataalamu wa kilimo,  ushirika,  ardhi, na ufugaji nyuki kutoka katika halmashauri  ya wilaya ya Mbarali na wataalamu wengine ni kutoka katika taasisi za fedha ikiwemo Benki ya CRDB na NMB.

MKURABITA imekuwa ikiowajengea uwezo wananchi kujikwamua kiuchumi kwa kuendesha mafunzo ya namna bora ya kutumia hatimiliki za kimila za kumiliki ardhi kijiletea maendeleo  ya kiuchumi na kijamii ili kuendana na dhamira ya Serikali ya Awamu ya Sita baada ya kurasimisha maeneo yao na kupatiwa hatimiliki hizo.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »