SERIKALI YA ZANZIBAR IMEAHIDI USHIRIKIANO NA WANAHABARI

Serikali ya awamu ya nane itaendelea kushirikiana na waandishi wa habari kwa kundoa vikwazo wanavyokabiliana navyo  katika upatikanaji wa taarifa kutoka taasisi za serikali. Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleima Abdulla ameleza hayo katika shughuli ya maadhimisho ya siku ya uhuru wa Habari duniani iliofanyika katika ukumbi wa Sheikh Idriss Abdul

Serikali ya awamu ya nane itaendelea kushirikiana na waandishi wa habari kwa kundoa vikwazo wanavyokabiliana navyo  katika upatikanaji wa taarifa kutoka taasisi za serikali.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleima Abdulla ameleza hayo katika shughuli ya maadhimisho ya siku ya uhuru wa Habari duniani iliofanyika katika ukumbi wa Sheikh Idriss Abdul Wakili uliopo Kikwajuni.

Ameleza kuwa serikali inathamini na kuunga mkono jitihada za waandishi wa habari nchini kutokana na kazi nzuri wanayifanya iliolenga kuimarisha weledi na uwajibikaji kwa viongozi wa watumishi wa umma katika sehemu zao za kazi.

Akizungumzia suala la kuzingatia maadili Makamu wa Pili wa Rais aliwatanabahisha waandishi  kwamba

Akiendelea na houtuba yake Makamu wa Pili wa Rais aliwakumbusha waandishi wa Habari kufuatilia na kuyafikia makundi yalio pembezoni kwa kusema..

Nae, Kaimu Waziri wa Habari, Utamuduni Sanaa na Michezo Mhe. Leila Mohamed Mussa aliwataka waandishi wa habari kutambua nafasi zao kwa kuzingatia utaalamu katika utendaji wao wa kazi ili kujitofautisha na watu wa kawaida.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Kamati ya wanahabari Zanzibar Farouk Karim  alisema Lengo kuu la kudhihirisha siku ya Uhuru duniani kwa upande wa Zanzibar ina lenga kuonesha kuwa vyombo vya habari vilivyopo nchini  vinafanya kazi kwa mashirikiano na serikali.

Katika maadhimisho hayo ya siku wa uhuru wa habari Duniani Mhe. Hemed aliwakabidhi tunzo waandishi waliofanya vizuri kupitia mashindano yalioandaliwa na Jumiya ya wanahabari na kusema tunzo hizo iwe chachu ya kuendeleza ubunifu zaidi na kuandika habari zenye tija katika Jamii.

Aidha Mhe. Hemed pamoja na tunzo zilizotolewa alipendekeza katika mashindano yajayo ingizwe tunzo maalum inayohusiana na masuala ya uwajibikaji akiahidi kulisimamia kwa nguvu zake zote.

Mwanahabari Salum Vuai wa Gazeti la Zanzibar leo na mwenzake Rehemu Juma Mema wa Hits FM wameibuka Washindi wa kwanza kwa kupata Tunzo ya Uandishi wa habari za Uchumi wa Buluu iliopewa jina Tunzo ya Dk. Hussein Ali Mwinyi

Tunzo  ya  Jenda na Jinsia iliopewa jina  Tunzo ya Mama Maryam Mwinyi imechukuliwa na Mwanahabari Wahida Nassor wa Hits FM wakati Tunzo ya uwajibikaji na kupinga vitendo vya Rushwa ilichukuliwa na Mwanahabari Sheha Salum Msabah kutoka Shirika la Utangazaji Zanzibar {ZBC}.

…………………………………

Kassim Abdi

Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar

Mei 30, 2021.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »