Wanafunzi 148,127 wachaguliwa kujiunga na kidato cha Tano na vyuo vya elimu na mafunzo ya ufundi

Wanafunzi 148,127 wachaguliwa kujiunga na kidato cha Tano na vyuo vya elimu na mafunzo ya ufundi

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Ummy Mwalimu amesema kuwa wasichana wote waliokidhi vigezo na kupata daraja la kwanza hadi la tatu wamechaguliwa kujiunga na kidato cha tano na vyuo vya elimu na mafunzo ya ufundi kwa mwaka 2021. Akiongea katika mkutano na waandishi wa habari leo

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Ummy Mwalimu amesema kuwa wasichana wote waliokidhi vigezo na kupata daraja la kwanza hadi la tatu wamechaguliwa kujiunga na kidato cha tano na vyuo vya elimu na mafunzo ya ufundi kwa mwaka 2021.

Akiongea katika mkutano na waandishi wa habari leo Jijini Dodoma wakati akitoa taarifa ya zoezi la uchaguzi wa wanafunzi wa kidato cha tano na vyuo vya elimu na mafunzo ya ufundi Waziri Ummy amesema jumla ya wanafunzi 148,127 wamekidhi vigezo wakiwemo wasichana 63,878 na wavulana 84, 249 sawa na asilimia 33.84 wamechaguliwa kujiunga na kidato cha tano na vyuo vya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kwa mwaka 2021.

Waziri Ummy amesema kuwa lengo la Serikali ni kuhakikisha inawainua wanawake ambapo kwa mwaka huu wanafunzi wasichana wote waliokidhi vigezo na kufaulu mitihani yao wamechaguliwa kujiunga na kidato cha Tano na Vyuo vya Elimu na Mafunzo ya Ufundi.

Ameendelea kufafanua kuwa wanafunzi 87,663 wakiwemo wasichana 41,885 na wavulana 45,778 sawa na asilimia 59.18 ya wenye sifa wamechaguliwa kujiunga na kidato cha tano katika shule 476 za Serikali zikiwemo shule mpya 42, wanafunzi wenye mahitaji maalum 288 sawa na asilimi 100 walikuwa na sifa ya kujiunga na kidato cha tano.

Vilevile, wanafunzi 41, 504 wakiwemo wasichana 17,646 na wavulana 23,858 sawa na asilimia 47.34 wamechaguliwa kujiunga na masomo ya tahasusi za Sayansi na Hisabati na wanafunzi 46,159 wakiwemo wasichana 24,239 na wavulana 21,920 sawa na asilimia 52.66 wamuchaguliwa kujiunga na tahasusi za masomo ya sanaa na biashara ambapo wanafunzi 1598 wamechaguliwa kujiunga na vyuo vya ufundi Arusha, Taasisi ya Teknolojia Dar-es-Salaam , Chuo cha Usimamizi wa Maendeleo ya Maji na Chuo cha Sanyansi na Teknolojia Mbeya.

Waziri Ummy ameendelea kufafanua kuwa idadi ya wanafunzi wenye sifa za kuchaguliwa kujiunga na kidato cha Tano na vyuo vya elimu ya ufundi imeongezeka kwa asilimia 14.07 kutoka 129,854 mwaka 2020 hadi 148,127 mwaka 2021 ikiwemo wasichana 63,878 ambao wamechaguliwa wote.

“Muhula wa kwanza wa masomo utaanza Mwezi Julai 5,2021 na atakayechelewa kuripoti watapangiwa wanafunzi wengine”amesema Mhe.Ummy

Sauti zote Na Barnabas Kisengi

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »