MAJALIWA: RAIS SAMIA AMEDHAMIRIA KUWALETEA WANANCHI MAENDELEO

MAJALIWA: RAIS  SAMIA AMEDHAMIRIA KUWALETEA WANANCHI MAENDELEO

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amewataka wananchi kuiunga mkono Serikali inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan kwa kuwa ina nia thabiti ya kuwaletea maendeleo. Ametoa kauli hiyo leo (Jumatatu Juni 7, 2021) wakati akizungumza kwa nyakati tofauti na wananchi wa kata za Nandagala, Likunja, Nambilanje na Ruangwa Mjini mkoa wa

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amewataka wananchi kuiunga mkono Serikali inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan kwa kuwa ina nia thabiti ya kuwaletea maendeleo.

Ametoa kauli hiyo leo (Jumatatu Juni 7, 2021) wakati akizungumza kwa nyakati tofauti na wananchi wa kata za Nandagala, Likunja, Nambilanje na Ruangwa Mjini mkoa wa Lindi.

Amesema Serikali ya Awamu ya Sita  inayoongozwa na Rais Samia imetoa Shilingi bilioni 1 kwa ajili ya ujenzi wa Sekondari katika kata ya Likunja ambayo itakuwa ni kubwa kuliko zote wilayani Ruangwa.

Aliongeza kuwa Shule hiyo itakuwa na madarasa 13, matundu ya vyoo 30, jengo la utawala , maabara 2 kubwa, mabweni 4,  nyumba za walimu 2, bwalo na jiko “pia vitajengwa viwanja vya michezo katika shule hiyo”.

Amesema Wilaya ya Ruangwa imedhamiria kuhakikisha inajenga shule za sekondari katika kata ambazo hazina shule hizo lengo likiwa ni kuhakikisha kwamba watoto wote wanapata fursa ya kusoma.

Kuhusu huduma ya maji safi na salama, Waziri Mkuu amesema Wizara ya Maji kupitia Wakala wa Maji Safi na Usafi wa Mazingira  Vijijini  (RUWASA)  imeanza kufanya usanifu wa mradi wa maji  kutoka eneo la Ndanda ambako kuna chanzo kikubwa cha maji cha Mbwinji ili kuyafikisha Ruangwa.

Amesema kuwa mradi huo utavinufaisha vijiji vya Mbecha, Michenga, Chimbira A na B, Nandagala, Namahema, Mpumbe, Nkowe, Mitoke na Likunja.

Akizungumzia sekta ya umeme, Waziri Mkuu amesema kazi ya usambazaji umeme vijijini na maeneo yaliyopo nje ya miji inaendeleavizuri na wale wote ambao wamelipia gharama za kuunganishiwa umeme wataunganishwa kupitia mpango wa REA.

Ameagiza kwamba  vijiji vyote ambavyo havijapatiwa na huduma ya umeme viunganishwe  kwa kuwa mkandarasi amekwishapatikana.

Pia, Waziri Mkuu amewataka wananchi kuanza kujenga maboma  ya ujenzi wa zahanati na yeye Mbunge wao atasaidia  upatikanaji wa mabati.

Kadhalika amesema kuwa Halmashauri ya wilaya ya Ruangwa  inakusudia kujenga Chuo cha Afya ambacho kitatoa mafunzo ya Uuguzi na wahudumu wengine wa sekta ya afya lengo likiwa ni kuongeza idadi ya watalamu wa afya.

Waziri Mkuu  Juni 8, 2021 anatarajia kufungua mashindano ya Shule za Msingi (UMITASHUMTA) na Shule za Sekondari  (UMISETA) katika uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara.

IMETOLEWA NA:

OFISI YA WAZIRI MKUU,

S. L. P. 980,

41193 – DODOMA,                      

JUMATATU, JUNI 7, 2021.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »