RC MPWAPWA AWATAKA WANANCHI KUZINGATIA SHERIA YA UHIFADHI WA MAZINGIRA

RC MPWAPWA AWATAKA WANANCHI KUZINGATIA SHERIA YA UHIFADHI WA MAZINGIRA

Na Barnabas Kisengi -Mpwapwa Mkuu wa wilaya ya Mpwapwa JABIR SHEKIMWER amewataka wananchi wa wilaya ya mpwapwa kuhakikisha wanatunza mazingira na kuacha tabia ya kukata kuni na kuchoma mikaa na kufanya shughuli za kibinadamu katika vyanzo vya maji wilayani hapo. Kauli hiyo ameitoa wakati wa ziara yake ya kukagua vyanzo vya maji wilayani mpwapwa  alipokuwa na

Na Barnabas Kisengi -Mpwapwa


Mkuu wa wilaya ya Mpwapwa JABIR SHEKIMWER amewataka wananchi wa wilaya ya mpwapwa kuhakikisha wanatunza mazingira na kuacha tabia ya kukata kuni na kuchoma mikaa na kufanya shughuli za kibinadamu katika vyanzo vya maji wilayani hapo. 
Kauli hiyo ameitoa wakati wa ziara yake ya kukagua vyanzo vya maji wilayani mpwapwa  alipokuwa na kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya kuangalia vyanzo vya maji na mazingira.


SHEKIMWER amesema kumekuwa na changamoto ya uharibifu wa mazingira katika baadhi ya maeneo kwa watu kufanya shughuli za kibinadamu katika vyanzo maji na ukataji wa kuni na kuchoma mikaa 
“kumekuwa na tabia ya baadhi ya wananchi wachache wamekuwa wakiharibu mazingira jambo ambalo linaleta mabadiliko ya tabia nchi ambapo watu wachache wamekuwa wakikata miti ovyo na wengine kuharibu vyanzo vya maji”


Mkuu wa wilaya amemwagiza afisa mazingira wa halimashauri ya wilaya ya mpwapwa kufanya tathimini ya uharibifu wa mazingira katika wilaya hiyo na kumwelekeza kuhakikisha anatumia sheria ndogo ndogo za halimashauri kuhakikisha kwa wale wanao haribu mazingira wanachukuliwa hatua za kisheria kufikishwa kwenye vyombo husika


“Hili jambo la uharibifu wa mazingira niliwekee msisitizo sana kwa afisa mazingira wa halimashauri ahakikishe anatumia Sheri ndogo ndogo za halimashauri kuhakikisha zinatumika pia ahakikishe anashirikiana na watendaji wa vijiji na wenyeviti wa vijiji na vitongoji kwakuwa wao ndio wako kwenye maeneo yao na wanawajua watu ambao wanatabia ya uharibifu wa mazingira”

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »