WAITARA ATAKA KASI UJENZI WA DARAJA LA KIYEGEA

WAITARA ATAKA KASI UJENZI WA DARAJA LA KIYEGEA

NAIBU Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mwita Waitara amesikitishwa na kitendo ujenzi wa daraja ya Kiyegea kufaniyika kwa kusuasua ambapo ameagiza Wakala wa Barabara(TANROADS)mkoa wa Morogoro kumpelekea taarifa ya ujenzi huo. Waitara alitoa agizo hilo juzi alipofanya ziara ya kushitukiza usiku kwa ajili ya kukagua ujenzi huo ambapo alisikitishwa na ujenzi huo ambao ulikuwa ukamilike

NAIBU Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mwita Waitara amesikitishwa na kitendo ujenzi wa daraja ya Kiyegea kufaniyika kwa kusuasua ambapo ameagiza Wakala wa Barabara(TANROADS)mkoa wa Morogoro kumpelekea taarifa ya ujenzi huo.

Waitara alitoa agizo hilo juzi alipofanya ziara ya kushitukiza usiku kwa ajili ya kukagua ujenzi huo ambapo alisikitishwa na ujenzi huo ambao ulikuwa ukamilike mwezi uliopita na kuiagiza Tanroad kumpelekea taarifa ya ujenzi kwa ujumla.

“Nimesikitishwa sana na ujenzi wa daraja hili sasa nimetoa agizo kwa Wakala wa Barabara(TANROADS) mkoa wa Morogoro kiniletea taarifa ofisini ikieleza ni lini ujenzi huu wa daraja la kiyegea ukakamilika kwani sioni sababu”alisema Waitara.

Naibu Waziri huo alisema kuwa haoni sababu za msingi daraja hilo kushindwa kukamilika kwa wakati tangu lilipo sombwa na maji mwezi Februari mwaka 2020 ambapo alimtaka Mkandarasi anayejenga daraja kuongeza kasi zaidi ya ujenzi.

Alisema mkoa Morogoro kuna miradi mingi yenye malalamiko kutokana na kushindwa kukamilika kwa wakati ikiwemo barabara ya Kidatu Ifakara ambapo alimtaka Meneja wa Tanroad kusimamia ujenzi huo ili kuepuka malalamiko.

“Ili kuweza kupepuka malalamiko mengi kutoka kwa wananchi wa mkoa huu ni wajibu wa Tanroad kuhakikisha wanafanya kazi usiku na mchana ili kuhakikisha barabara zote zinapikika bila kuwa na changamoto yoyote ile”alisema Waitara.

Mbali na hilo pia aliitaka Tanroad mkoa huo kuhakikisha miradi yote wanayoisimamia inakamilika kwa wakati ambapo alisema kuwa mtumishi yeyote atakayeonesha uzemba wowote hatamchekea bali atamchukulia hatua.

Kwa upande wake Mhandisi Msimamizi wa mradi wa ujenzi wa daraja hilo la Kiyegea Brown Kisamo alisema kuwa ujenzi huo unakwenda vizuri na kwamba baada ya wiki hii kukamilika kutakuwa na hatua kubwa itakatokuwa imefikiwa.

Aidha Mhandisi Brown alisema baadhi ya changamoto zinazokabili ujenzi huo zitatatuliwa ambapo alimuhakikisia Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi kuwa ujenzi huo mbali na kuchelewa kukamilika lakini zoezi linafanyika vizuri sana.

Daraja la Kiyegea ilililopo mpakani mwa wilaya ya Kilosa Na Gairo lilikatika mwanzoni mwa mwaka jana ambapo kwa wakati huo Rais Hayati Magufuli alifika eneo hilo na kujionea athari zilizipo ambapo alitoa maagizo kwa Wizara husika.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »