BABU TALE ATOA MILIONI 40 KUSAIDIA MIUNDOBNU YA ELIMU JIMBONI

BABU TALE ATOA MILIONI 40 KUSAIDIA MIUNDOBNU YA ELIMU JIMBONI

OFISI ya mbunge wa jimbo la Morogoro kusini mashariki imetoa milioni 40.05 kutoka katika mfuko wa jimbo ili kukamilisha vyumba vya madarasa 16 katika shule za sekonda 9 zilizopo katika jimbo hilo Hatua imekuja katika kuunga mkono jitihada za serikali katika kukabiliana na uhaba wa vyumba vya madarasa nchini ambapo katika shule hizo wananchi walianza

OFISI ya mbunge wa jimbo la Morogoro kusini mashariki imetoa milioni 40.05 kutoka katika mfuko wa jimbo ili kukamilisha vyumba vya madarasa 16 katika shule za sekonda 9 zilizopo katika jimbo hilo

Hatua imekuja katika kuunga mkono jitihada za serikali katika kukabiliana na uhaba wa vyumba vya madarasa nchini ambapo katika shule hizo wananchi walianza kwa kujitolea nguvu kazi zao mpaka kufikia hatua ya umaliziaji

Hayo yalibainishwa jana na afisa mipango halmashauri ya Morogoro, Salifa Venace, wakati wa ziara ya kamati ya mfuko wa jimbo hilo ya kukagua utekelezaji wa miradi ya maendeleo ambayo imefikiwa na fedha hizo

Alisema miongoni wa shule ambazo zimepatiwa fedha hizo ni pamoja na shule ya sekondari ya Gwata, Mikese, Nelson Mandela, Kiroka, Mkuyuni, Tegetero na Kinole

“fedha hizo zimetuunga mkono katika umaliziaji wa shule za sekindari zetu 16 ambazo wananchi walianza kuzijenga kwa kutumia nguvu zao, tunatarajia katika kipindi hiki cha likizo madarasa haya yatakuwa yamekamilika na kuanza kutumika baada ya shule kufunguliwa ili kuondoa msongaano wa wanafunzi wengi darasa moja” alisea

 Hatujuani Ally ni afisa elimu sekondari halashauri ya Morogoro alisema kuwa kasi ya ujenzi imekuwa kubwa baada ya kupata fedha za umaliziaji wa madarasa hayo ambapo pia inaenda sambamba na ukamilishaji wa madarasa ya wanafunzi wa kidato cha tano na sita

Alisema katika halmashauri hiyo jumla ya shule sita zitakuwa na kidato cha tano na sita ambapo kwa upande wa jimbo la Morogoro kusini mashariki kutakuwa na shule tatu za sekondari Ngerengere, Nelson Mandela na Mkuyuni ambazo zote zipo katika hatua za mwisho kwaajili ya kupokea

Alisea kwa upande wa Morogoro kusini shule zilizotengwa kuwa na kidato cha tano na sita ni pamoja na sekondari ya Matombo ambayo tayali walishaanza kutoa elimu hiyo, huku shule nyingine ni Bwakila Chini na Mvua ambazo ujenzi wake utaanza hivi karibuni.

“tunashukuru ofisi ya mbunge kutoa fedha hizi za mfuko wa jimbo na kuzielekeza katika sekta ya elimu hasa katika kufanikisha kupata madarasa kwaajili ya kidato cha tano na sita ambapo itatoa fulsa kwa wanafunzi wengi kuendelea masomo ya juu” alisema Hatujuani

Kwa upande wake diwani wa kata ya Tegetero  Yusuph Ngoba,  alisema pamoja na ukamilishaji wa vyumba vya madarasa serikali inapaswa pia kutupia jicho katika ujenzi wa mabweni kwaajili ya watoto wa kike ambao wamekuwa wakilazimika kutembea umbali refu

Alisema kwa sasa baadhi ya shule katika halmashauri hiyo zimekuwa zikitukia mfumo wa kuweka kambi kwa wanafunzi wa kidato cha nne ili wapate muda wa kujisomea lakini hiyo haitosho ni muhimu kupatikana kwa mabweni kwaajili ya wanafunzi wote.

ReplyForward
Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »