WABUNGE WATAKIWA KUWA MABALOZI KUELIMISHA WANANCHI UMUHIMU WA SENSA 2022

WABUNGE WATAKIWA KUWA MABALOZI KUELIMISHA WANANCHI UMUHIMU WA SENSA 2022

Na Barnabas Kisengi-Dodoma  Serikali kupitia ofisi ya waziri mkuu sera,uratibu,bunge,kazi,vijana,ajira na wenye ulemavu imewataka wa wabunge wa bunge wa jamhuri  ya muungano wa Tanzania hususani wanawake kwenda kuwa mabalozi wa utoaji elimu kwa wananchi na kuhamasisha watanzania kijitokeza kushiriki kwa wingi katika zoezi la uandikishaji wa sensa ya watu na makazi mwakani 2022. Rai hiyo

Na Barnabas Kisengi-Dodoma 

Serikali kupitia ofisi ya waziri mkuu sera,uratibu,bunge,kazi,vijana,ajira na wenye ulemavu imewataka wa wabunge wa bunge wa jamhuri  ya muungano wa Tanzania hususani wanawake kwenda kuwa mabalozi wa utoaji elimu kwa wananchi na kuhamasisha watanzania kijitokeza kushiriki kwa wingi katika zoezi la uandikishaji wa sensa ya watu na makazi mwakani 2022.

Rai hiyo imetolewa  leo Jijini Dodoma na Waziri Wa Nchi Ofisi Ya Waziri Mkuu Sera,Uratibu,Bunge,Kazi,Vijana,Ajira Na Wenye Ulemavu BI JENISTA MHAGAMA katika mafunzo ya waheshimiwa wajumbe wa umoja wa wabunge wanawake Tanzania(TWPG) kuhusu ukokotoaji wa Takwimu yaliyoa andaliwa na ofisi ya taifa Takwimu.

Kwa upande wake Naibu Spika Wa Bunge La Tanzania DKT.TULIA ACKSON amesema kuwa mafunzo hayo yatawasaidia wabunge uwezo wa kutoa michango yao bungeni kuhusu maendeleo ya wananchi.

Naye Mtakwimu Mkuu Wa Serikali BI ALBINA CHUWA akaeleza kuwa ofisi hiyo imejipanga kutumia mfumo wa kielekitronic katikakuandikisha sensa ya watu na makazi ya 2022 ili kuepuka changamoto ambazo zilijitokeza mwaka 2012.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »