SERIKALI KUPINGA VIKALI UKATILI DHIDI YA WAZEE

SERIKALI KUPINGA VIKALI UKATILI DHIDI YA WAZEE

Na Barnabas Kisengi-Dodoma  KATIKA kuhakikisha ulinzi na usalama kwa wazee wote hapa nchini unaimarika, serikali inaratibu utekelezaji wa mkakati wa kitaifa wa kutokomeza mauaji ya wazee 2018/ 2019 – 2022- 2023, ikiwa ni pamoja na kuhakikisha ulinzi na usalama wa wazee wasiojiweza na ambao hawana watu wa kuwatunza huku serikali  ikiendelea  kusimamia matunzo katika makazi

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Dorothy Gwajima akizungumza na Waandishi wa Habari (Hawapo pichani) kuhusu Siku ya Kimataifa ya kupinga Ukatili dhidi ya Wazee, Jijini Dodoma leo.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Dorothy Gwajima akizungumza na Waandishi wa Habari (Hawapo pichani) kuhusu Siku ya Kimataifa ya kupinga Ukatili dhidi ya Wazee, Jijini Dodoma leo. Kulia ni Kamishna wa Ustawi wa Jamii nchini Dkt. Naftali Ng’ondi.

Na Barnabas Kisengi-Dodoma 

KATIKA kuhakikisha ulinzi na usalama kwa wazee wote hapa nchini unaimarika, serikali inaratibu utekelezaji wa mkakati wa kitaifa wa kutokomeza mauaji ya wazee 2018/ 2019 – 2022- 2023, ikiwa ni pamoja na kuhakikisha ulinzi na usalama wa wazee wasiojiweza na ambao hawana watu wa kuwatunza huku serikali  ikiendelea  kusimamia matunzo katika makazi ya wazee.

Akitoa tamko  kwa Waandishi wa Habari,Leo Jijini Dodoma  kuelekea siku ya Kimataifa ya kupinga ukatili dhidi ya wazee ,Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii jinsia wazee na watoto Dkt, Doroth Gwajima amesema Serikali imeendelea kuzitambua  familia masikini wakiwemo wazee na kuwawezesha kupata mahitaji ya msingi.

Amesema kwa mujibu wa Ibara ya 14 ya katiba ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 inatambua haki ya msingi ya kuishi ambapo inasema kila mtu anahaki ya kuishi na kpata kutoka kwa jamii hifadhi ya maisha yake kwamujibu wa sheria Ibara ya 16 ya katiba inayotambua haki ya ulinzi wa nafsi yake

Aidha ametoa rai kwa wale wote ambao wamekuwa wakiwaza kuendelea kufanya vitendo vya ukatili kwa wazee ikiwemo ukatili wa kimwili, kihisia na kiuchumi wajue kuwa mkono wa sheria ni mrefu na sheria itachukua mkondo wake kikamilifu pindi wakibainika wamefanya vitendo hivyo

Kaulimbiu ya siku ya Kimataifa ya kupinga ukatili dhidi ya wazee inasema ‘’tupaze sauti kupinga ukatili dhidi ya wazee’’

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »