Dar Yaendelea Kuwa Tishio UMITASHUMTA Mkoani Mtwara

Dar Yaendelea Kuwa Tishio UMITASHUMTA Mkoani Mtwara

IKIWA leo ni Siku ya Nne tangu kufunguliwa kwa mashindano ya UMITASHUMTA na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb) ufunguzi uliofanyika kwenye uwanja wa Nangwanda Sijaona Mkoani Mtwara, timu ya Mkoa wa Dar es Salaam imeendelea kuwa tishio kwenye mashindano hayo kwa kupata ushindi Mkubwa katika michezo mbalimbali

IKIWA leo ni Siku ya Nne tangu kufunguliwa kwa mashindano ya UMITASHUMTA na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb) ufunguzi uliofanyika kwenye uwanja wa Nangwanda Sijaona Mkoani Mtwara, timu ya Mkoa wa Dar es Salaam imeendelea kuwa tishio kwenye mashindano hayo kwa kupata ushindi Mkubwa katika michezo mbalimbali waliyokwisha kucheza hadi kufikia jioni ya leo ya tarehe 11 Juni, 2021.

Mapema siku ya leo timu ya Mkoa wa Dar es Salaam waliweza kuifunga timu ya Mkoa wa Pwani kwa seti 3-0 katika mchezo wa mpira wa wavu (wasichana) na kisha kuifunga timu ya Mkoa wa Arusha kwa seti 3 -0 katika mchezo wa Mpira wa Wavu (wavulana).

Aidha, katika mechi zilizoendelea kuchezwa siku ya leo, tarehe 11 Juni, 2021 timu ya Dar es Salaam imeweza kupata ushindi wa magoli 3 – 0 kwa kuifunga timu ya Mkoa wa Kagera katika mchezo wa mpira wa miguu (Wavulana), na pia ikapata ushindi wa goli 1-0 kwa kuwafunga Tabora mchezo wa mpira wa miguu (Wasichana).

Halikadhalika, timu ya Dar es Salaam imeweza kupata ushindi wa magoli 19-4 kwa kuwafunga Njombe kwenye mchezo wa mpira wa mikono (Wavulana).

Mchezo mwengine walioweza kushinda Dar es Salaam hii leo ni mchezo wa Netiboli walipowafunga magoli 26-6 timu ya Rukwa.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Translate »