MAKAMU WA RAIS ASHIRIKI IBADA MAALUM YA KULIOMBEA TAIFA JIJINI DODOMA

MAKAMU WA RAIS ASHIRIKI IBADA MAALUM YA KULIOMBEA TAIFA JIJINI DODOMA

NA PENDO MANGALA,DODOMA. MAKAMU wa Rais, Dkt Philip Mpango ameshiriki ibada Maalum ya kuliombea Taifa Jijini Dodoma huku akisema Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan itahakikisha inaongoza nchi kwa kuzingatia maadili,uadilifu, misingi ya sheria na utawala bora kwa lengo la kujenga uchumi imara wenye ushindani kwa maslahi ya umma. Dkt

NA PENDO MANGALA,DODOMA.

MAKAMU wa Rais, Dkt Philip Mpango ameshiriki ibada Maalum ya kuliombea Taifa Jijini Dodoma huku akisema Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan itahakikisha inaongoza nchi kwa kuzingatia maadili,uadilifu, misingi ya sheria na utawala bora kwa lengo la kujenga uchumi imara wenye ushindani kwa maslahi ya umma.


Dkt Mpango ametoa kauli hiyo leo wakati wa ibada hiyo Maalum ya kuliombea Taifa iliyoandaliwa na Taasisi ya Kingdom Leadership Network Tanzania (KLNT)ambapo amesema dhamira hiyo itatekelezwa kwa kuzingatia Mpango wa Tatu wa Maendeleo ya Taifa wa Miaka Mitano (2021/22-2025/26) ambao umesisitiza utawala bora wenye kuzingatia sheria kama msingi wa maendeleo ya Taifa.

Sambamba na hilo ameishukuru KLNT kuwakutanisha viongozi wa dini, wanasiasa na wananchi kufanya ibada maalum kwa taifa na serikali itahakikisha ushirikiano huo unafanyika kwa maendeleo yenye usawa.


Kwa upande wake Mwenyekiti wa Taasisi ya KLNT Dokta Fredrick Ringo, ameeleza dhumuni la mkusanyiko huo ni kuliombea Taifa haaa viongozi kwqkufuata utawala bora kwa misingi ya sheria na kuwaomba wanasiasa kuwa waadilifu katika kutekeleza ahadi wanazotoa kwa wananchi huku Mbunge wa Viti Maalum Sophia Mwakagenda akieleza umuhimu wa wanasiasa kuishi na ahadi wanazozitoa kwa wananchi.


 

Kwa upande wake  Dk.Charles Sokile ambaye ni Mkuu wa Chuo cha biashara cha Joseph  na ni Mkurugenzi wa mahusiano ya kimataifa wa Taasisi hiyo ya Kingdomleadership ameeleza umuhimu wa wafanyabiashara kulipa kodi na kuzingatia maadili katika shughuli zao.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »