MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI AWATAKA MAWAKILI KUJIENDELEZA KIELIMU

MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI AWATAKA MAWAKILI KUJIENDELEZA KIELIMU

Na Barnabas Kisengi-Dodoma  MWANASHERIA  Mkuu wa Serikali, Profesa Adelardus Kilangi,amewataka Mawakili wa Serikali Nchini kuendelea kujielimisha kila siku kutokana na kukua kwa taaluma ya Sheria Ulimwenguni kulingana na umuhimu wa  kazi yao wanayoifanya ili kuongeza ufanisi katika utendaji kazi. Profesa Kilangi ametoa wito huo  Jijini hapa wakati akifungua mafunzo ya siku nne kwa Mawakili wa Serikali

Mwanasheria  Mkuu wa Serikali, Prof. Adelardus Kilangi
Wakili Mkuu wa Serikali,Gabriel Malata

Na Barnabas Kisengi-Dodoma 

MWANASHERIA  Mkuu wa Serikali, Profesa Adelardus Kilangi,amewataka Mawakili wa Serikali Nchini kuendelea kujielimisha kila siku kutokana na kukua kwa taaluma ya Sheria Ulimwenguni kulingana na umuhimu wa  kazi yao wanayoifanya ili kuongeza ufanisi katika utendaji kazi.

Profesa Kilangi ametoa wito huo  Jijini hapa wakati akifungua mafunzo ya siku nne kwa Mawakili wa Serikali yenye lengo  la kuwaongezea uwezo katika stadi za uendeshaji madai ya usuluhishi kwa kuwapa ujuzi ambayo yameandaliwa na  Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali.

Amebainisha kuwa  mafunzo hayo ni muhimu na yatasaidia kuwanoa Mawakili hao ili kuendana na mabadiliko ya taaluma ya Sheria ambayo yamekuwa yanatokea kila siku ulimwenguni.

Sambamba na hilo amesema Mafunzo hayo yataongeza uwezo na weledi katika suala zima la usuluhishi la madai mbalimbali huku akiitaka Ofisi ya Wakili wa Serikali kushirikiana na Taasisi mbalimbali katika kutatua changamoto  mbalimbali zinazoikabili  hiyo  ikiwemo uhaba wa mawakili wa Serikali.

Kwa upande wake Wakili Mkuu wa Serikali,Gabriel Malata amesema ofisi hiyo ilipewa jukumu lakuendesha madai ya kesi ndani nan je ya nchi na kupitia mafunzo hayo yanaenda kuwaweka katika mtazamo mmoja wa uendeshaji wa mashauri kwaniaba ya Serikali na Taasisi zake huku akibainisha mafanikio na changamoto mbalimbali.

Nao baadhi ya Mawakili wa Serikali  wamesema kuwa matarajio yao makubwa ni kuongezea ujuzi wa namna yakuweza kufanya kazi zao kwa ustadi mkubwa na kuzingatia maadili ya taaluma yao.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »