RC MAKALLA ATANGAZA KIAMA KWA WEZI WA MAFUTA KIGAMBONI.

RC MAKALLA ATANGAZA KIAMA KWA WEZI WA MAFUTA KIGAMBONI.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Amos Makalla leo ametangaza Vita na Mtandao wa wezi wa mafuta ghafi kupitia bomba kuu la mafuta Kigamboni na kulielekeza Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es salaam kuwashughulikia kikamilifu wezi hao ambapo adi leo Jumla ya watuhumiwa 15 wanashikiliwa. RC Makalla amesema hayo wakati wa

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Amos Makalla leo ametangaza Vita na Mtandao wa wezi wa mafuta ghafi kupitia bomba kuu la mafuta Kigamboni na kulielekeza Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es salaam kuwashughulikia kikamilifu wezi hao ambapo adi leo Jumla ya watuhumiwa 15 wanashikiliwa.

RC Makalla amesema hayo wakati wa ziara ya kukagua miundombinu ya Kupokea Mafuta ghafi kutoka kwenye Meli za Mafuta adi kwenye Visima ambapo ameshuhudia uharibifu mkubwa wa miundombinu uliofanywa na Mkazi mmoja aliechimba handaki adi kwenye Bomba kuu la mafuta na kujiunganishia Jambo lililopelekea hasara ya upotevu wa Mafuta kwa Wafanyabiashara.

Aidha RC Makalla amejionea namna Mkazi huyo alivyokuwa akiyapakia Mafuta hayo ya wizi kwenye Magari makubwa ya kubeba kokoto na mchanga ambayo ndani yake yamefungwa matank makubwa ya Mafuta na juu zinapangwa kokoto ili kuwazuga watu.

Kutokana na Wizi huo RC Makalla ameeleza kutoridhishwa na maelezo aliyopewa na TPA na Wakala wa uagizaji Mafuta kwa pamoja na kuamua kuhitisha kikao Cha pamoja Siku ya Jumatatu kwenye ukumbi wa Anatoglo kitakachojumuisha Waagizaji Mafuta, TPA, TRA na Wadau wote wa Mafuta ili wajadili namna bora ya kuhakikisha tatizo hilo halijirudii na kupitia mikataba yao hususani kipengele Cha namna gani mfanyabiashara aliepokea Mafuta pungufu tofauti na Yale aliyolipia anafidiwa.

Wakati huohuo RC Makalla amefanya kikao Cha pamoja na Baraza la Madiwani na Watendaji Wilaya ya Kigamboni ambapo amewapatia viaombele ikiwemo utatuzi wa kero za Wananchi, suala la usafi, ukusanyaji wa Mapato, usimamizi wa miradi ya maendeleo, ulinzi na usalama na Mambo mengine.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »