TANZANIA YAENDELEA KUSHIKA NAFASI YA 10 BORA KWENYE UTALII BARA LA AFRIKA

TANZANIA YAENDELEA KUSHIKA NAFASI YA 10 BORA KWENYE UTALII BARA LA AFRIKA

NA MWANDISHI WETU, WINDHOEK, NAMIBIA. TANZANIA imeendelea kung’ara ndani ya Bara la Afrika kwa kutangaza vyema vivutio vyake vya Utalii ambapo imeweza kuwa miongoni mwa nchi  10 bora kwa mwaka wa tatu mfululizo, kuanzia 2017 hadi  2020.Ripoti hiyo imetolewa mapema leo  kwenye mkutano wa Kimataifa wa Utalii wa Kanda ya Afrika ulioandaliwa na Shirika la

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Damas Ndumbaro akizungumza katika mkutano wa Kimataifa wa Utalii wa kanda ya Afrika ulioandaliwa na Shirika la  Umoja wa Mataifa la Utalii (UNWTO) unaofanyika kwa muda wa siku tatu katika Jiji la Windhoek nchini Namibia. Kupitia mkutano huo Tanzania  imepata fursa ya kushirikiana na Jumuiya ya Kimataifa hususan viongozi wa Serikali na wadau wa utalii kutoka nchi wanachama wa UNWTO katika kukabiliana na athari za COVID-19 na kuandaa mikakati madhubuti ya kurejesha sekta ya utalii katika hali ya awali.
 Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Damas Ndumbaro (katikati) akiwa na baadhi ya washiriki mbalimbali wa  mkutano wa Kimataifa wa Utalii wa kanda ya Afrika ulioandaliwa na Shirika la  Umoja wa Mataifa la Utalii (UNWTO) unaofanyika kwa muda wa siku tatu katika Jiji la Windhoek nchini Namibia wakifuatilia wasilisho la lenye lengo la  kuimarisha utangazaji wa vivutio vya utalii vilivyopo Bara la Afrika ikizingatiwa kuwa Tanzania ni miongoni mwa nchi zenye vivutio vingi na vya kipekee katika Bara hili. Kushoto ni Kamishna Msaidizi Maendeleo ya Biashara kutoka Shirika la Hifadhi za Taifa, Beatrice Kessy
Baadhi ya Washiriki kutoka nchi  mbalimbali za Afrika wakifuatilia  mkutano wa Kimataifa wa Utalii wa kanda ya Afrika ulioandaliwa na Shirika la  Umoja wa Mataifa la Utalii (UNWTO) wakifuatilia wasilisho la lenye lengo la  kuimarisha utangazaji wa vivutio vya utalii vilivyopo Bara la Afrika katika kipindi hiki cha ugonjwa wa UVIKO 19 ambao umeathiri sekta ya utalii duniani kote kwa kiasi kukibwa.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Damas Ndumbaro akIfuatilia  mkutano wa Kimataifa wa Utalii wa kanda ya Afrika ulioandaliwa na Shirika la  Umoja wa Mataifa la Utalii (UNWTO) ulioanza kufanyika kuanzia jana  tarehe 14 Juni,  2021 katika Jiji la Windhoek nchini Namibia. Kupitia mkutano huo Tanzania yatajwa kufanya vizuri katika masuala ya utalii licha ya uwepo wa changamoto wa ugonjwa wa COVID – 19
 Baadhi ya Washiriki kutoka nchi mbalimbali  za Afrika wakifuatilia  mkutano wa Kimataifa wa Utalii wa kanda ya Afrika ulioandaliwa na Shirika la  Umoja wa Mataifa la Utalii (UNWTO) wakifuatilia wasilisho la lenye lengo la  kuimarisha utangazaji wa vivutio vya utalii vilivyopo Bara la Afrika katika kipindi hiki cha ugonjwa wa UVIKO 19 ambao umeathiri sekta ya utalii duniani kote kwa kiasi kukibwa
Kamishna Msaidizi Maendeleo ya Biashara, Beatrice Kessy  kutoka Hifadhi za Taifa (TANAPA)  akizungumza wakati wa  Mkutano wa Kimataifa wa Utalii wa Kanda ya Afrika ulioandaliwa na Shirika la  Umoja wa Mataifa la Utalii (UNWTO) ambapo amesema Tanzania ni miongoni mwa nchi zenye vivutio vingi na vya kipekee Barabi Afrika ambapo ameomba ushirikiano wa makampuni makubwa ya Kimataifa kuisaidia Tanzania  kutangaza vivutio vya utalii vilivyoko Tanzania ili viweze kujulikana na watu wengi duniani ili kuongeza idadi ya watalii wataokatembelea Tanzania , Mkutano huo  unaofanyika kwa muda wa siku tatu katika Jiji la Windhoek nchini Namibia.  
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Damas Ndumbaro akifanya  kikao cha ana kwa ana mbobezi  wa kimataifa wa kutangza vivutio vya Utalii kutoka Shirika la Umoja wa Kimataifa  la Utalii ( UNWTO) Bi. Olgo Nowak mara baada ya kufanya  wasilisho lake lengo la kuzijengea uwezo nchi za Afrika kutangaza vivutio vya utalii vilivyoko Afrika  kupitia mitandao ya kijamii ambapo Tanzania imetajwa kung’ara kumi bora kwa nchi za  Afrika kwa kutangaza vivutio vyake vya utalii kwa muda wa miaka mitatu mfululizo kuanzia mwaka 2017 hadi mwaka 2020. Kushoto ni Kamishna Msaidizi Maendeleo ya Biashara kutoka Shirika la Hifadhi za Taifa, Beatrice Kessy
Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Damas Ndumbaro akizungumza na Balozi wa Tanzania nchini Namibia, Mhe.Modestus Kipilimba wakati alipowasili kwa ajili ya kushirikia mkutano wa Kimataifa wa Utalii kanada ya Afrika uliondaliwa na Shirika la Umoja wa Kimataifa la Utalii (UNWTO) unaofanyika kwa uda wa siku tatu nchini Namibia ambapo Tanzania ikiwa kama nchi mwanachama wa UNWTO itapata fursa ya kutoa maoni yetu kwa lengo la kuimarisha utangazaji wa vivutio vya utalii vilivyopo Bara la Afrika ikizingatiwa kuwa Tanzania ni miongoni mwa nchi zenye vivutio vingi na vya kipekee katika Bara hili. 




NA MWANDISHI WETU, WINDHOEK, NAMIBIA.


TANZANIA imeendelea kung’ara ndani ya Bara la Afrika kwa kutangaza vyema vivutio vyake vya Utalii ambapo imeweza kuwa miongoni mwa nchi  10 bora kwa mwaka wa tatu mfululizo, kuanzia 2017 hadi  2020.
Ripoti hiyo imetolewa mapema leo  kwenye mkutano wa Kimataifa wa Utalii wa Kanda ya Afrika ulioandaliwa na Shirika la Kimataifa la Utalii  Duniani  (UNWTO), Mtaalamu wa utangazaji wa Utalii, Bi. Olga Nowak aliitangaza Tanzania kushika nafasi ya saba  ambayo inakuwa ni mara ya tatu.

Katika mkutano huo, Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Damas Ndumbaro akiwa ameambatana na Watalaamu wake kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii wanashiriki  ambapo Waziri Dkt. Ndumbaro amesema Tanzania imejaliwa kuwa na vivutio vingi na vya kipekee ambavyo havipatikani mahali popote duniani isipokuwa Tanzania

Katika kumi bora hiyo,   Afrika ya Kusini imetajwa kushika nafasi ya kwanza  ikifutiwa na nchi ya  Misri  katika utangazaji vyema  ya vivutio vyake vya  utalii.

Aidha katika ripoti hiyo, Tanzania imetajwa  kuendelea kuongoza na kufanya vizuri katika sekta ya utalii licha ya uwepo wa changamoto wa ugonjwa wa UVIKO19  ambao umeikumba karibu Mataifa mbalimbali duniani kote.


Tanzania imekuwa na vivutio mbalimbali vinavyotamba Duniani ikiwemo mlima mrefu barani Afrika, Mlima Kilimanjaro, Hifadhi zenye vivutio vikubwa vya Wanyama kama Hifadhi ya Serengeti, Hifadhi ya Nyerere, Hifadhi ya Ruaha, Tarangile,l pamoja na Mamlaka ya Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro

Katika hatua nyingine  Tanzania kushiriki katika mkutano huo kupitia Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Ndumbaro na wataalamu  imepata fursa ya kushirikiana na Jumuiya ya Kimataifa hususan viongozi wa Serikali na wadau wa utalii kutoka nchi wanachama wa UNWTO katika kukabiliana na athari za COVID-19 na kuandaa mikakati madhubuti ya kurejesha sekta ya utalii katika hali ya awali kwa kufanya vikao vya ana kwa ana na viongozi wanaoshiriki mkutano huo

Pia, Tanzania imepata  fursa ya kutoa maoni yake kwa lengo la kuimarisha utangazaji wa vivutio vya utalii vilivyopo Bara la Afrika ikizingatiwa kuwa Tanzania ni miongoni mwa nchi zenye vivutio vingi na vya kipekee katika Bara la Afrika ambapo Waziri Dkt. Ndumbaro amemkaribisha Mtaalamu wa masuala ya utangazaji kuja Tanzania kutoa ujuzi huo.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »