ASILIMIA 16 YA WATU WENYE UMRI YA ZAIDI YA MIAKA60 WAMEPATA MANYANYASO YA KISAIKOLOJIA.

ASILIMIA 16 YA WATU WENYE UMRI YA ZAIDI YA MIAKA60 WAMEPATA MANYANYASO YA KISAIKOLOJIA.

Na Barnabas Kisengi-Dodoma  Imeelezwa kuwa asilimia 16 ya watu wenye umri zaidi ya miaka 60 wamepata manyanyaso ya kisaikolojia, (11.6%), kiuchumi (6.8%), kutokujaliwa (4.2%),na kimwili (2.6%). Hayo yamebainishwa jijini Dodoma Juni 15,2021  na  kamishna wa Tume ya Haki za Binadamu na utawala bora Dkt Fatma Khalfani katika Maadhimisho ya Siku ya Kupinga Ukatili dhidi ya

Na Barnabas Kisengi-Dodoma 

Imeelezwa kuwa asilimia 16 ya watu wenye umri zaidi ya miaka 60 wamepata manyanyaso ya kisaikolojia, (11.6%), kiuchumi (6.8%), kutokujaliwa (4.2%),na kimwili (2.6%).

Hayo yamebainishwa jijini Dodoma Juni 15,2021  na  kamishna wa Tume ya Haki za Binadamu na utawala bora Dkt Fatma Khalfani katika Maadhimisho ya Siku ya Kupinga Ukatili dhidi ya Wazee Duniani kwa niaba ya  mwenyekiti wa Tume hiyo Jaji Mstaafu Mathew Mwaimu  ambapo hiyo ni Kwa mujibu wa takwimu za Shirika la Afya Duniani (WHO) .

Amesema Katika baadhi ya nchi na jamii mbalimbali wazee wanakabiliwa na changamoto mbalimbali.

Hivyo amebainisha kuwa ,Tume inatoa wito kwa Wananchi wote kuachana na vitendo vyote vya ukatili dhidi ya wazee ambapo hatua hii ni muhimu katika kutekeleza kauli mbiu ya maadhimisho hayo kitaifa inayosema “Paza Sauti Kupinga Ukatili dhidi Wazee.”

Dkt Fatma  ameendelea kufafanua kuwa Katika kutekeleza suala hili nchini, Ibara ya 12 (2) na Ibara ya 14 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 pamoja na marekebisho yake, zimeeleza juu ya wazee kupewa heshima na kupata hifadhi kutoka kwa jamii wanamoishi.

Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora inaisihi Serikali, wadau na jamii kukamilisha kutunga Sheria ya Wazee ili kurahisisha utekelezaji wa Sera ya Wazee ya mwaka 2003,Wadau na Jamii kuendeleza kutoa elimu ya haki za binadamu na utawala bora kwa wananchi wote,Serikali iendelee kuboresha huduma za afya kwa jamii, na huduma hizo zitolewe bure kwa makundi maalumu ikiwemo wazee wote, ikiwa ni pamoja na kukamilisha mpango wa bima ya afya kwa wote;

Serikali kupitia vyombo vya ulinzi na usalama ihakikishe panakuwepo ulinzi madhubuti kwa wazee ikiwa ni pamoja na kuwakamata wahusika wa mauaji ya wazee na kuwafikisha katika vyombo vya dola

Kwa mujibu wa sensa ya watu na makazi ya mwaka 2002, Tanzania ilikuwa na wazee 1,952,041 (sawa na wanaume 940,229 na wanawake 1,011,812) na katika sensa ya mwaka 2012 idadi ya wazee iliongezeka hadi kufikia 2,507,568 (wanaume 1,200,210 na wanawake 1,307,358) sawa na 5.6% ya wananchi wote.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »