Na Barnabas Kisengi-Dodoma Ikiwa leo Juni 16,2021 bara la Afrika likiadhimisha siku ya Mtoto wa Afrika,Mkuu wa Wilaya ya Dodoma mjini Mwalimu Josephat Maganga amesema suala la mtoto kutokwenda shule ni uzembe wa mzazi pamoja na mlezi ,hivyo amehimiza walezi ,wazazi ,kamati za shule pamoja na jamii kwa ujumla kulipa kipaumbele suala la elimu ili mtoto aweze
Na Barnabas Kisengi-Dodoma
Ikiwa leo Juni 16,2021 bara la Afrika likiadhimisha siku ya Mtoto wa Afrika,Mkuu wa Wilaya ya Dodoma mjini Mwalimu Josephat Maganga amesema suala la mtoto kutokwenda shule ni uzembe wa mzazi pamoja na mlezi ,hivyo amehimiza walezi ,wazazi ,kamati za shule pamoja na jamii kwa ujumla kulipa kipaumbele suala la elimu ili mtoto aweze kupata haki ya elimu.
Mwalimu Maganga amebainisha hayo leo Juni 16 ,2021 jijini Dodoma katika maadhimisho ya siku ya Mtoto wa Afrika ambapo kiwilaya yamefanyika katika kata ya Kilimani ambapo amesema ni wajibu kwa wadau kuja kwa pamoja kutekeleza kuhakikisha kila mtoto anakwenda shule.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora nchini Tanzania Jaji Mstaafu Mathew Mwaimu amesema jukumu la malezi ya mtoto katika msingi wa maadili na mahitaji mengine ni la mzazi.
Nao baadhi ya Watoto waliohudhuria katika maadhimisho hayo akiwemo Joyce Frank,Licia Saduka pamoja na Sabuli Said wamesema siku ya Mtoto wa Afrika ina umuhimu mkubwa katika utetezi wa haki zao
Chimbuko la siku ya mtoto wa Afrika ni kumbukumbu ya watoto zaidi ya 2000 waliuawa wakati wakiandamana kupinga ubaguzi wa rangi katika mfumo wa elimu nchini Afrika kusini mnamo mwaka 1976 ambapo kauli mbiu ya mtoto wa Afrika 2021 ni’’Tutekeleze ajenda ya mwaka 2040 kwa Afrika inayolinda haki za mtoto’’.
Leave a Comment
Your email address will not be published. Required fields are marked with *