WAFANYAKAZI NCHINI KOTE WAMETAKIWA KIJIUNGA NA VYAMA VYA WAFANYAKAZI.

WAFANYAKAZI NCHINI KOTE WAMETAKIWA KIJIUNGA NA VYAMA VYA WAFANYAKAZI.

SERIKALI imewataka waajiri wote hapa nchini kuwaruhusu wafanyakazi wao kujiunga na vyama vya wafanyakazi ili kuleta tija katika suala zima la uwajibikaji na pia kusaidia kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili wafanyakazi wao. Hayo yalisemwa mwishoni mwa wiki iliyopita  na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Ummy Hamisi ambapo alisema kitendo cha wafanyakazi kujiunga na vyama

SERIKALI imewataka waajiri wote hapa nchini kuwaruhusu wafanyakazi wao kujiunga na vyama vya wafanyakazi ili kuleta tija katika suala zima la uwajibikaji na pia kusaidia kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili wafanyakazi wao.

Hayo yalisemwa mwishoni mwa wiki iliyopita  na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Ummy Hamisi ambapo alisema kitendo cha wafanyakazi kujiunga na vyama vya wafanyakazi kutapunguza changamoto na kufungua fursa mbali mbali.

“Napenda kutumia nafasi hii kuwataka waajiri wote nchini kuwapa fursa wafanyakazi kujiunga katika vyama ili kupunguza migogoro kwani kutawapa fursa ya kutambua haki zao za msingi kupitia vyama vyao hivyo”alisema Ummy.

Naibu Waziri huyo alisema kuwa kuwapa fursa wafanyakazi kujiunga katika vyama kupunguza migogoro na kwamba kutawapa fursa ya kutambua haki zao za msingi kutokana na uwepo wa vyama hivyo maeneo mbalimbali hapa nchini.

Alisema kuwa serikali imekuwa ikifanya jitihada mbalimba ili kuhakikisha wafanyakazi wote nchini wanakuwa katika mazingira mazuri katika utendaji wao wa makujumu lakini baadhi ya watu wamekuwa wakikwamisha juhudi hizo.

Aidha alisema kuwa serikali itahakikisha inakuwa karibu na wafanyakazi wote hapa nchini ikiwa ni pamoja na waajiri wao ambapo aliwataka waajiri kuhakikisha wafanyakazi wao wanajiungua na vyama vya wafanyakazi ili kuleta tija kwa taifa.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama Cha Wafanyakazi wa Viwanda,Biashara,Taasisi za Kifedha Huduma na Ushaturi(TUICO) taifa Paul Sangeze alisema chama chake kitaendelea kushirikiana na serikali.

Mwenyekiti huyo alisema kuwa ushirikano wa serikali uliopo umekuwa ukiwafanya wafanyakazi kuijamina na kutekeleza majukumu yao imasavyo na kwamba changamoto zilizipo ana uhakika zitatuliwa haraka iwezekanavyo.

Aidha aliipongeza serikali kwa kutoa agizo kwa waajiri kuhakikisha kuwa wafanyakazi wao wote wanajiunga na vyama vya wafanyakazi ambapo alisema kuwa yeye kama kiongozi wa TUICO atahakikisha agizo hilo linatekelezeka.

Nao wajumbe wa Baraza Kuu TUICO taifa walisema ipo dhana kwa baadhi ya waajiri kupinga vyama hivyo ambapo walitoa wito kwa viongozi wa vyama vya wafanyakazi hapa nchini kuwa na weledi ili kuongeza imani kwa wafanyakazi.

Karim Hussein ni Katibu TUICO Morogoro alisema uadilifu wa viongozi wa TUICO kutawagengea imani wafanyakazi kitendo kitakachowashawishi wengi kujiunga mbapo aliahidi kuendelea kufanya majukumu yake kwa uaminifu.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »