IDADI YA WATOTO WENYE UDUMAVU YATISHA MOROGORO

IDADI YA WATOTO WENYE UDUMAVU YATISHA MOROGORO

KATIKA Mkoa wa Morogoro watoto wapatao laki moja kati ya watoto laki nne walio na umri chini ya miaka mitano wanakabiliwa na udumavu, idadi inayotajwa kupungua kutokana na mpango mkakati wa serikali wa kutokomeza tatizo la udumavu hapa Nchini. Wakati jitihada za serikali kwa kushirikiana na wadau wa masuala ya lishe zikiendelea kwa kutoa elimu

KATIKA Mkoa wa Morogoro watoto wapatao laki moja kati ya watoto laki nne walio na umri chini ya miaka mitano wanakabiliwa na udumavu, idadi inayotajwa kupungua kutokana na mpango mkakati wa serikali wa kutokomeza tatizo la udumavu hapa Nchini.

Wakati jitihada za serikali kwa kushirikiana na wadau wa masuala ya lishe zikiendelea kwa kutoa elimu kwa jamii wakilenga kundi la watoto chini ya miaka mitano, wakina mama wajawzito na vijana rika balehe bado baadhi yao wanakwamisha jitihada hizo kutokana na uelewa duni wa masuala ya lishe.

Afisa Lishe Mkoa wa Morogoro Salome Magembe akizungumza wakati wa kikao cha tathimini ya shughuli za mradi wa lishe endelevu, alisema takwimu hizo zimefikiwa kutokana na uelewa duni wa wananchi.

Alisema kwamjibu wa tafiti za mwaka 2015 hadi 2016 Mkoa wa Morogoro ulikuwa na watoto waliodumaa asilimia 33.4 hadi kufikia asilimia 26.4 mwaka 2018 ambapo licha ya kushuka kiasilimia, kwa namba mkoa huo una watoto zaidi ya laki moja wenye udumavu.

“pamoja na kushuka kwa asilimia lakini bado tunaona kwa idadi tuna watoto wengi ambapo kuna watoto takribani 106,730 walio duma kati ya watoto 400,000 wa chini ya miaka mitano” alisema Salome

Aidha Afisa huyo wa lishe alisema mradi wa lishe endelevu umesaidia kupunguza udumavu kwa watoto mkoani humo kwa kuwafikia wananchi wengi kupitia kwa vikundi vya wakulima na wafugaji wa mfano kupitia watendaji wa serikali kuanzia ngazi ya mtaa, kijiji, kata na Halmashauri za Wilaya pamoja na wahudumu wa afya ngazi ya jamii.

Alisema wananchi wamehamasishwa kulima mazao yenye virutubisho ikiwemo kilimo cha mbogamboga na matunda yanoyokomaa kwa muda mfupi, kufuga wanyama wadogowadogo kama sungura kwa ajili ya kujipatia kitoweo sambamba na wakina Baba kushiriki vyema kusimamia lishe kwenye familia zao.

‘tunashukuru kwa uwepo wa mradi japo unaelekea ukingoni lakini tumeona matunda yake, wananchi wamehamasishwa kulima mazao yenye virutubisho pamoja na ufugaji wa sungura na tumeshuhudia wakina Baba nao wakishiriki kusimamia lishe” alisema Salome

Kwa upande wake Meneja wa Mradi wa Lishe endelevu Mkoa wa Morogoro Nuhu Yahya alisema matarajio yao ni kuona serikali inaendeleza zoezi la utoaji wa elimu ya lishe bora kwa wananchi ambao hawatafikiwa na mradio pindi utakapo koma.

Alisema mradi huo umefanikiwa kuwafikia wahudumu wa afya 239 ili kutoa elimu kupitia kliniki ya Baba, mama na mtoto, wakulima wa mfano waliofikiwa 247 na wakulima wa mashamba darasa 4388 huku wakina mama 265 wakipokea mafunzo ya lishe, lengo elimu hiyo ya lishe isibakie kwa maafisa lishe pekee bali iwafikie walengwa.

“tunatajia kuona serikali inaendeleza utoaji elimu ya lishe bora kwa wananchi ambao hawatafikiwa na mradio pindi utakapo koma, tumefanikiwa kuwakia wakulima na wafugaji wa mfano kama ilivyoelezwa pamoja na akina mama, lengo elimu hiyo ya lishe isibakie kwa maafisa lishe pekee” alisema Nuhu

Naye Mkuu wa kitengo cha kilimo na mifugo Anania Yusto alieleza zaidi ya vikundi 39 wamevipatiwa mifugo ya kufuga ikiwemo Kuku, Sungura na Samaki ambapo vikundi viwili kati ya hivyo vikipewa shamba darasa la mazo ya msimu ambayo ni mahindi na maharage.

Kikaoa cha tathimini ya shughuli za mradi wa lishe endelevu umekutanisha wakuu wa idara mbalimbali kutoka Halmashauri tisa za Mkoa wa Morogoro pamoja na wadau wa masuala ya lishe uliolenga kujadili namna gani serikali itakavyosimamia utoaji elimu kwa wananchi baada ya muda wa mradi kumalizika

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »