RC MAKALLA AWANUSURU WANANCHI NA ATHARI ZA MAZINGIRA.

RC MAKALLA AWANUSURU WANANCHI NA ATHARI ZA MAZINGIRA.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Amos Makalla leo amepatia ufumbuzi kilio Cha wakazi wa Kilungule Wilaya ya Temeke waliokumbwa na adha ya Vumbi na udongo unaotokana na Ujenzi unaoendelea wa Daraja la kuunganisha Kata ya Kilungule na Buza linalogharimu Shilingi bilioni 12 ambapo ameagiza Wakazi hao kutafutiwa nyumba za kuishi kwa wakati

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Amos Makalla leo amepatia ufumbuzi kilio Cha wakazi wa Kilungule Wilaya ya Temeke waliokumbwa na adha ya Vumbi na udongo unaotokana na Ujenzi unaoendelea wa Daraja la kuunganisha Kata ya Kilungule na Buza linalogharimu Shilingi bilioni 12 ambapo ameagiza Wakazi hao kutafutiwa nyumba za kuishi kwa wakati huu Ujenzi unaendelea kwa mustakabali wa Afya zao.

RC Makalla ametatua Mgogoro huo wakati wa ziara ya kukagua miradi ya Ujenzi wa Barabara za DMDP Wilaya ya Temeke na msafara wake kusimamishwa na Wakazi hao ambapo baada ya kuwasikiliza ameelekeza baada ya kumalizika kwa Ujenzi huo Manispaa ya Temeke iangalie Kiusalama Kama Kuna uwezekano wa Wananchi hao kuendelea kuishi au walipwe Fidia wakatafute maeneo mengine.

Hayo yamejiri wakati wa ziara ya ukaguzi wa miradi ya Ujenzi wa Barabara za DMDP Wilaya ya Temeke.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »