RC MAKALLA ATAKA WAKANDARASI KUKAMILISHA MIRADI KWA WAKATI.

RC MAKALLA ATAKA WAKANDARASI KUKAMILISHA MIRADI KWA WAKATI.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Amos Makalla amewataka Wakandarasi wanaotekeleza miradi ya Ujenzi wa Barabara za DMDP Wilaya ya Temeke kuhakikisha miradi hiyo inakamilika kwa wakati ili kutatua changamoto za Wananchi. RC Makalla ametoa maelekezo hayo wakati wa ziara ya kutembelea na kukagua miradi ya Ujenzi wa Barabara, Madaraja na Mitaro ambayo

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Amos Makalla amewataka Wakandarasi wanaotekeleza miradi ya Ujenzi wa Barabara za DMDP Wilaya ya Temeke kuhakikisha miradi hiyo inakamilika kwa wakati ili kutatua changamoto za Wananchi.

RC Makalla ametoa maelekezo hayo wakati wa ziara ya kutembelea na kukagua miradi ya Ujenzi wa Barabara, Madaraja na Mitaro ambayo Ujenzi wake umekuwa ukisuasua na kuleta usumbufu kwa Wananchi ambapo amewataka Wakandarasi waliokuwa wameondoka kwenye maeneo ya kazi Kutokana na kucheleweshewa malipo warudi na kuendelea na kazi wakati anashughulikia malipo yao.

Miongoni mwa Barabara alizotembelea RC Makalla na ujenzi wake umekuwa ukisuasua ni Barabara ya Clinic mbagala yenye thamani ya Bilioni 2.2, Barabara ya Msikitini yenye urefu wa mita 375, Barabara ya Kizingha urefu wa mita 975m na thamani ya Bilioni 1.087, Barabara ya Bughudadi bilioni 1.4 na Mwera inayogharimu bilioni 1.4 na kuagiza Barabara hizo kukamilika kwa wakati na kwa Ubora.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Translate »