WAZIRI GWAJIMA AWAPA SOMO MAKATIBU AFYA

WAZIRI GWAJIMA AWAPA SOMO MAKATIBU AFYA

 NA MWANDISHI-MOROGORO WAZIRI wa Wizara ya afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dokta Dorothy Gwajima amewataka makatibu wa afya kote Nchini kuwajibika kikamilifu kwenye majukumu yao kwa kusimamia kikamilifu rasilimali zilipo kwenye vituo vyao vya kazi. Waziri Gwajima alisema hayo kwenye mkutano wa makatibu afya kutoka Halmashauri na mikoa yote Nchini uliofanyika Mkoani

 NA MWANDISHI-MOROGORO

WAZIRI wa Wizara ya afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dokta Dorothy Gwajima amewataka makatibu wa afya kote Nchini kuwajibika kikamilifu kwenye majukumu yao kwa kusimamia kikamilifu rasilimali zilipo kwenye vituo vyao vya kazi.

Waziri Gwajima alisema hayo kwenye mkutano wa makatibu afya kutoka Halmashauri na mikoa yote Nchini uliofanyika Mkoani Morogoro, uliolenga kujadili na kutatua changamoto zinazoikabili kada hiyo, alisema kusuakusua kwa utendaji kwa baadhi ya makatibu kunazorotesha kada hiyo.

Aliwaeleza makatibu hao kuachana na tabia ya uzembe kwa kutotekeleza majukum yao ipasavyo kwa kutengeneza sababu zisizo na mashiko ikiwemo kutofikia vituo vya afya kwenye halamshauri zao kwa madai ya kutowezeshwa usafiri badala yake waombe kujaziwa mafuta huku akiwasisitizia kuzingatia miundo yao ya kazi kwa kuandaa taarifa sahihi.

“labda niwaeleze fanyeni kazi tekelezeni majukum yenu ipasavyo, tabia ya kutojituma kwenye kazi na kuanza ooh sikuvifikia vituo usafiri hakuna, hela hakuna kama unaona hela hakuna omba ujaziwe mafuta, ikishindika hata vituo vyenye umbali wa kilometa tano kwanini hamfikii, wajibikeni kikamilifu” alisema Gwajima

Pia Waziri huyo alisema anatambua kada ya makatibu afya ni miongoni mwa sekta zisizo na bodi ya kusimamia uwajibikaji na utendaji kazi na kwamba mganyo huo wa majukum ndio ambao umeifanya serikali ione umhimu wake huku akiagiza kuundwa bodi na baraza litakalosimamia kada hiyo

“natambua nyinyi ni miongoni mwa kada za afya ambazo mpaka sasa hazijapata bodi na baraza kama wizara tunalichukua hili, naagiza njooni mchukue mkataba muunde bodi na baraza litakalowasaidia, ukiangalia kwa makini makatibu wa afya ndio watendaji wakuu” alisema Gwajima

Kwa upande Mwenyekiti wa Chama cha Makatibu wa Afya Tanzania (AHSATA} Daniel Muhochi alisema chama hicho ni kiungo mhimu kwa wizara ya afya na kwamba kinakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo kukosekana idara inayowaunganisha na wizara husika.

Alisema moja ya changamoto ni kukosekana kwa idara kwenye wizara ya afya inayowaunganisha na chama hicho ambapo baadhi ya changamoto zinzowasilishwa wizarani wakati mwingine hufanyiwa kazi na mtu ambaye hana uelewa zaidi kuhusiana na kada hiyo.

“tangu kuanzishwa kwa kada hii mwaka 1975 wizarani hakuna idara ambayo inayotuanganisha moja kwa moja na hili jambo linafanya sasa kama ni changamoto zinweza zikapelekwa na wakati mwingine zikashugulikiwa na mtu ambaye hana uwelewa na kada hii” alisema Muhochi

Naye Mkuu wa Wilaya ya Mvomero Albinus Mgonya alisema serikali inatambua mchango wa sekta hiyo na kwamba imetoa miongozo kama ilivyoainishwa kwenye sheria za utumishi wa umma, ambapo kwa kada ya afya wamesisitizwa kuzingatia kutoa huduma bora kwa wananchi, utii kwa serikali, kufanya kazi kwa bidii na weledi na kila mtumishi kuongeza thamani ya shughuli za Halmashauri yake

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »