KATIBU MKUU WA UNWTO ARIDHIA OMBI LA TANZANIA KUWA MWENYEJI WA MKUTANO UJAO WA UTALII BARA LA AFRIKA

KATIBU MKUU WA UNWTO ARIDHIA OMBI LA  TANZANIA KUWA MWENYEJI WA MKUTANO UJAO WA UTALII BARA LA AFRIKA

Na Mwandishi Wetu, Windhoek, Namibia. Katibu Mkuu wa SHIRIKA la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Masuala ya Utalii (UNWTO), Zurab Pololikashvil ameridhia ombi la Tanzania kuwa  kuwa mweyeji wa mkutano ujao wa masuala ya Utalii Bara la Afrika  Hatua hiyo inakuja kufuatia kikao cha ana kwa kilichofanyika pembeni baina ya Waziri wa Maliasili na Utalii, Damas

Na Mwandishi Wetu, Windhoek, Namibia.

Katibu Mkuu wa SHIRIKA la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Masuala ya Utalii (UNWTO), Zurab Pololikashvil ameridhia ombi la Tanzania kuwa  kuwa mweyeji wa mkutano ujao wa masuala ya Utalii Bara la Afrika 

Hatua hiyo inakuja kufuatia kikao cha ana kwa kilichofanyika pembeni baina ya Waziri wa Maliasili na Utalii, Damas Ndumbaro na Katibu Mkuu huyo wa UNWTO, Zurab Pololikashvil katika Mkutano wa Kimataifa wa Utalii wa Kanda ya Afrika uliofanyika kwa muda wa siku tatu Jijini Windhoek nchini Namibia.

Aidha, Dkt. Ndumbaro amesema  mbali ya kuridhia ombi la Tanzania kuwa Mwenyeji wa mkutano wa Utalii mwakani, Pia Katibu huyo pia amekubali yeye mwenyewe binafsi kutembelea Tanzania na kuonana na viongozi mbalimbali wa Kitaifa pamoja na wadau wa utalii kwa ajili ya kufanya maongezi juu ya mustakabali wa Utalii  baada ya UVIKO 19.

amesema mbali ya kupata fursa ya kufanya mikutano ya ana kwa ana na wadau mbalimbali moja kati ya wadau hao ni Katibu Mkuu ambaye anayeshughulikia masuala ya Utalii wa Umoja wa Mataifa, ambaye amekubali mkutano ujao wa Utalii Barani Afrika, ufanyikie Tanzania’’. Alisema Mhe. Ndumbaro.

Mhe. Ndumbaro ameongeza kuwa, Katibu huyo pia amekubali yeye mwenyewe binafsi kutembelea Tanzania na kuonana na viongozi mbalimbali wa Kitaifa pamoja na wadau wa utalii kwa ajili ya kufanya maongezi juu ya mustakabali wa Utalii  baada ya UVIKO 19.

Akizungumza Waziri Dkt. Damasi Ndumbaro amesema Ujumbe wa Tanzania umeweza kupata faida hizo mbalimbali  sambamba na kupata uzoefu mkubwa ikiwemo pia kutangaza fursa za Utalii za Tanzania katika mkutano huo ambao una wadau wakubwa wa Utalii.

Aidha, Waziri Dkt. Ndumbaro amesema kikao cha ana kwa ana kwa ana kimeleta mafanikkio ambapo Katibu Mkuu huyo amekubaliwa ombi la kuiingiza Tanzania kuwa  moja kati ya nchi tatu Barani Afrika ambazo zitapata mradi wa Umoja wa Mataifa kwenye masuala ya Utalii. 

Amesema Tanzania itakuwa miongoni mwa  nchi tatu zitakazonufaika na mradi huo ambapo Namibia na Cape Vede  zimeshaingizwa toka zamani .

”Kwetu sisi kama Tanzania kwa namna ya kipekee  tumepewa upendeleo mkubwa sana wa kuingizwa katika mradi huo ambao mbali ya kunufaisha sekta ya watalii bali itaweza kuongeza ajira kwa viaja kupitia sekta ya utalii…’’. Alisema Mhe. Ndumbaro.

  Akizungumzia faida za mktano huo, Dkt. Ndumbaro amesema  mkutano huo umewakutanisha mawaziri wa UItaliii kumi na tao kutoka nchi 15 ambapo  wamejadili mambo mengi, wamebadilishana uzoefu mkubwa ikiwa pamoja na kupata mawasilisho mbalimbali kutoka kwenye makampuni  yenye uwezo wa juu kabisa wa kutangaza utalii duniani.  

Aidha, Waziri Dkt. Ndumbaro amesema Ujumbe wa Tanzania katika mkutano huo umepata utaalam na uzoefu mkubwa kwa jinsi gani watakavyoweza kunasuka na ugonjwa huo wa UVIKO 19, amewapongeza watanzania kushiriki na kuweza kufanikiwa.

Katika hatua nyingine,  Waziri Dkt. Ndumbaro amesema kupitia uzoefu wa mkuatano huo ambao umemalizi kufanyika nchini Namibia, Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii inatarajia kufanya mkutano  wa Kimataifa wa  Utalii na Masoko utakaofanyika mwezi Oktoba mwaka huu Jijini Arusha.

Katika mkutano huo , Dkt. Ndumbaro amesema watalaamu wabobezi wa kutoka makampuni makubwa duniani wanaojihusisha na kutangaza vivutio vya utalii  wamealikwa kushiriki kupitia mwaliko wa kvikao vya ana kwa ana alivyovifanya  na  Watalamu hao  kwa nyakati tofauti wakati wa mkutano wa Kimataifa wa Utalii ulipokuwa ukiendelea.

Amesema mkutano huo utafanyika kwa muda wa siku tatu ambapo Wataala,mu na Wadau wa Utalii watapata fursa ya kujadili mikakati na mbinu za kukuza sekta utalii nchini ikiwa na pamoja na kuona namna ya kujikwamua katika kipindi kigumu hiki cha ugojwa wa UVIKO 19 ulivyodumuza Utalii

HABARI KATIKA PICHA

 

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Damas Ndumbaro (kulia) akifanya kikao cha ana kwa ana na Katibu Mkuu wa Shirika la Umoja wa Kimataifa linaloshughulikia Masuala ya Utalii (UNWTO) Zurab Pololikashvili (kushoto)  pembeni mwa  Mkutano wa Kimataifa wa Utalii wa Kanda ya Afrika ulioandaliwa na Shirika la Umoja wa Kimataifa la Utalii (UNWTO)   ambapo Katibu Mkui hiuyo  ameridhia ombi la  Tanzania kuwa mweyeji wa mkutano ujao wa masuala ya Utalii Barani Afrika ambapo Tanzania imeingia kuwa miongoni mwa nchi  tatu za Afrika zitakazowezeshwa kunufaiaka na  mradi mkubwa wa masuala ya Utalii.unaofadhiliwa na UNWTO.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Damas Ndumbaro (kulia) akimkabidhi zawadi mbalimbali kutoka Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA)  Katibu Mkuu wa Shirika la Umoja wa Kimataifa linaloshughulikia Masuala ya Utalii (UNWTO) Zurab Pololikashvili (kushoto)  mara baada  kufanya kikao cha ana kwa ana pembeni  katika Mkutano wa Kimataifa wa Utalii wa Kanda ya Afrika ulioandaliwa na Shirika la Umoja wa Kimataifa la Utalii (UNWTO)   ambapo Ktibu Mkuu huyo  ameridhia ombi la  Tanzania kuwa mweyeji wa mkutano ujao wa masuala ya Utalii Barani  Afrika na pia ameiingiza Tanzania kuwa miongoni  mwa nchi ya tatu za Afrika  zitakazowezeshwa mradi mkubwa wa masuala ya Utalii.unaofadhiliwa na UNWTO. Mkutano huo ulianza Juni 14, 2021 Jijini Windhoek nchini Namibia na  una lengo la kukabiliana  na athari za UVIKO 19 na kuandaa mikakati madhubuti ya kurejesha sekta ya utalii katika hali ya awali.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Damas Ndumbaro (kulia) akimkabidhi moja ya  zawadi ya Kitabu kinachoelezea maeneo yalihifadhiwa  ambayo yanasimamiwa na  Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) kwa   Katibu Mkuu wa Shirika la Umoja wa Kimataifa linaloshughulikia Masuala ya Utalii (UNWTO) Zurab Pololikashvili (kushoto)  mara baada  kufanya kikao cha ana kwa ana.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Damas Ndumbaro (kulia) akimkabidhi moja ya  zawadi ya seti ya vikombe vyenye nembo ya   Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA)  Katibu Mkuu wa Shirika la Umoja wa Kimataifa linaloshughulikia Masuala ya Utalii (UNWTO) Zurab Pololikashvili (kushoto)  mara baada  kufanya kikao cha ana kwa ana mara baada ya kufunguliwa rasmi kwa  Mkutano wa Kimataifa wa Utalii wa Kanda ya Afrika ulioandaliwa na Shirika la Umoja wa Kimtaifa la Utalii (UNWTO) ambapo ameridhia ombi la  Tanzania kuwa mweyeji wa mkutano ujao wa masuala ya Utalii Barani  Afrika ambapo pia ameiingiza Tanzania kuwa miongoni mwa nchi tatu za Afrika zitakayowezeshwa mradi mkubwa wa masuala ya Utalii.unaofadhiliwa na UNWTO. Mkutano huo ulianza Juni 14, 2021 Jijini Windhoek nchini Namibia na  una lengo la kukabiliana  na athari za UVIKO 19 na kuandaa mikakati madhubuti ya kurejesha sekta ya utalii katika hali ya awali.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Damas Ndumbaro (kulia) akipeana mkono na  Katibu Mkuu wa Shirika la Umoja wa Kimataifa linaloshughulikia Masuala ya Utalii (UNWTO) Zurab Pololikashvili (kushoto)  mara baada  kufanya kikao cha ana kwa ana mara ikiwa ni ishara ya kumshukuru  kwa kuridhi ombi la  Tanzania kuwa mweyeji wa mkutano ujao wa masuala ya Utalii Barani  Afrika ambapo pia ameiingiza Tanzania kuwa miongoni mwa nchi ya tatu za Afrika zitakazowezeshwa mradi mkubwa wa masuala ya Utalii.unaofadhiliwa na UNWTO. Mkutano huo ulianza Juni 14, 2021 Jijini Windhoek nchini Namibia na  una lengo la kukabiliana  na athari za UVIKO 19 na kuandaa mikakati madhubuti ya kurejesha sekta ya utalii katika hali ya awali.
Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »