MAWAZIRI WA SADC WAPITISHA ITAFAKI KUENDELEZA UTALII

MAWAZIRI WA SADC WAPITISHA ITAFAKI KUENDELEZA UTALII

Na Barnabas Kisengi-Dodoma  Mawaziri wa Nchi Wanachama ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika SADC wamepitisha itifaki ya kuendeleza utalii ili kuongeza mchango wa sekta  ya utalii katika uchumi wa nchi za SADC. Itifaki hiyo itaimarisha shughuli za utangazaji wa utalii na hivyo kuongeza idadi ya watalii wanaotembelea Nchi za SADC. Hayo yamebainishwa leo Jijini

Na Barnabas Kisengi-Dodoma 

Mawaziri wa Nchi Wanachama ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika SADC wamepitisha itifaki ya kuendeleza utalii ili kuongeza mchango wa sekta  ya utalii katika uchumi wa nchi za SADC.

Itifaki hiyo itaimarisha shughuli za utangazaji wa utalii na hivyo kuongeza idadi ya watalii wanaotembelea Nchi za SADC.

Hayo yamebainishwa leo Jijini Dodoma na Naibu Waziri Wizara ya Maliasili na Utalii Mh Mary Masanja wakati akitoa taarifa kwa vyombo vya Habari kuhusu mkutano wa Mawaziri wa SADC wanaohusika na Mazingira,Maliasili na Utalii uliofanyika kwa njia ya mtandao.

Aidha,amesema Mawaziri wa SADC wametumia fursa hiyo ya mkutano kuhimiza nchi wanachama kuridhia itifaki ya SADC ya usimamizi wa Mazingira kwaajili ya kujenga maendeleo endelevu.

Wakati huo huo,Masanja amesema mkutano umejadili Mkakati wa SADC wa mabadiliko ya Tabia ya nchi na Mpango kazi wa utkelezaji wake ,hivyo Nchi wanachama zimehimizwa kuutekeleza mpango kazi huo na kuarifiwa kuhusu kuanzishwa kwa mkakati maalumu wa wataalamu (Thematic Working Group) kwaajili ya kuratibu masuala ya mabadiliko ya Tabia ya nchi pamoja na kupunga athari za manufaa.

Katika kuhakikisha uhifadhi wa matumizi endelevu wa rasilimali misitu,Mawaziri wa Nchi Wanachama wa SADC wamepitisha mkakati wa Misitu wa SADC wa miaka kumi (2020-2030),kupitia mkakati huo Nchi wanachama watakuza uwezo wa Taasisi zinazosimamia rasilimali za misitu,kukuza na kusimamia soko la biashara ya mazao ya misitu,kuchochea uwekezaji wa kifedha na ushiriki wa sekta binafsi na kuimarisha ulinzi na uongoaji wa maeneo ya misitu yaliyoharibiwa.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Translate »