Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Kata ya Sandali Manispaa ya Temeke Jijini Dar es Salaam wamepongeza uteuzi wa Wakuu wa Wilaya za Tanzania Bara uliyofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan hapo jana Juni 19, 2021. Hayo yamebainishwa na Katibu wa Umoja wa Vijana wa Chama

Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Kata ya Sandali Manispaa ya Temeke Jijini Dar es Salaam wamepongeza uteuzi wa Wakuu wa Wilaya za Tanzania Bara uliyofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan hapo jana Juni 19, 2021.
Hayo yamebainishwa na Katibu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Kata ya Sandali Manispaa ya Temeke Bwana Mrisho Kamba alipozungumza na Waandishi wa Habari mapema leo juni 20, 2021.

Bwana Mrisho Kamba amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kuwaamini Vijana na kuwateuwa kwa uwingi na kuahidi kutoa ushirikiano kwa Mkuu wa Wilaya hiyo mteule , Jokate Mwegelo.
“Tunamshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kumteua Dada yetu Jokate Mwegelo kuwa Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Jokate Mwengelo ni Mchapakazi hodari tangu alipokuwa Katibu Hamasa Chipukizi Taifa, na alipokuwa Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, tunampenda tunamkaribisha Temeke tunamuahidi ushirikiano” alisema Bwana Mrisho Kamba.
Kwa upande Katibu Hamasa wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) wa kata hiyo, Bwana Omary Yusuph, amesema wana matumaini makubwa kwa Vijana walioteuliwa kufanya kazi wa weledi.

Bwana Omary ametumia fursa hyo kuwasihi Vijana wote nchini kuendelea kuwa na subira kwani Rais Samia Suluhu Hassan aliahidi kuwateua vijana wengi zaidi kushika nyadhifa mbalimbali kwa kuzingitia utendaji kazi wao.
Kwa ujumla wao Viongozi wa UVCCM Kata ya Sandali wamewasihi Vijana wote na Wakuu wa Wilaya wateule kote nchini kutobweteka bali wafanye kazi kwa juhudi zao zote ili kuliwezesha Taifa la Tanzania kuwa na Uchumi Mkubwa zaidi.
Leave a Comment
Your email address will not be published. Required fields are marked with *