MCH. MWANKENJA: KUPIMA AFYA SI UDHAIFU WA IMANI.

MCH. MWANKENJA: KUPIMA AFYA SI UDHAIFU WA IMANI.

Na Emesto Eliudy, Dar ES Salaam. Kanisa la Moravian Tanzania Jimbo la Mashariki likishirikiana na Kituo Cha kutoa Huduma za Afya cha DSB POlyclinic limeendesha Semina ya Afya iliyoambatana na zoezi la Upimaji Afya Bure kwa waumini wake na Watanzania kwa ujumla. Akizungumuza katika kanisa la Moravian Ushirika wa Tabata Liwiti uliopo Jijini Dar ES

Na Emesto Eliudy, Dar ES Salaam.


Kanisa la Moravian Tanzania Jimbo la Mashariki likishirikiana na Kituo Cha kutoa Huduma za Afya cha DSB POlyclinic limeendesha Semina ya Afya iliyoambatana na zoezi la Upimaji Afya Bure kwa waumini wake na Watanzania kwa ujumla.


Akizungumuza katika kanisa la Moravian Ushirika wa Tabata Liwiti uliopo Jijini Dar ES Salaam lilipofanyika zoezi hilo, Mwenyekiti wa Wilaya ya Kusini, Mch. Bwigane Mwakalinga, Alisema kuwa lengo la Semina hiyo ni kuwasaidia waumini wa kanisa Hilo kujua na kutambua umuhimu wa kutunza afya zao.


“Tumeandaa tukio hili kwa lengo la kusaidia waumini mbalimbali kupima na kusikiliza maelezo ya wataalamu juu ya Afya zao ili kuwa na Afya njema. Tunaamini kanisa lililo salama ni kanisa ambalo Lina watu ambao Wana Afya njema kwani Jambo la Afya linatuhusu sote. Hivyo nawasihi Watanzania wote Upimaji wa Afya ni Jambo la maana Sana katika maisha yetu ya kila siku”. Alisema Mch. Bwigane.

Mwenyekiti wa Kanisa la Moravian Tanzania Jimbo la Mashariki Wilaya ya Kusini, Mch. Bwigane Mwakalinga

Kwa Upande wake Makamu Mwenyekiti wa Jimbo hilo, Mch. Timothy Mwankenja alisema kuwa Wakristo wengi wanashindwa kwenda kupima Afya zao wakidhani kuwa kufanya hivyo ni udhaifu wa Imani zao huku akihimiza waumini wa kanisa Hilo kuwa na utamaduni wa kupima Afya zao Mara kwa Mara.


“Inafika Mahali tunaokoka tunapitiliza, unafikiri kupima Afya yako ni udhaifu wa Imani. Wako watu hawaendi hospitali wakidai kuwa Wana maagano na Mungu wao, hizo ni Imani potofu. Mungu ndiye aliyewaweka madaktari, Kama hufahamu madaktari ni watumishi wa Mungu, wapo ili walitumikie kusudi la Bwana ili kuangalia Afya zetu, ni muhimu Sana kupima Afya zetu. Kupima Afya si udhaifu wa Imani. Alisema Mch. Mwankenja.

Makamu Mwenyekiti wa Kanisa la Moravian Tanzania Jimbo la Mashariki, Mch. Timothy Mwankenja.


Naye Daktari Bingwa wa Magonjwa ya ndani, Dkt. Basla Tumaini Aliwataka Watanzania kutambua kuwa Kuna magonjwa amabayo hayaonyeshi dalili za awali mpaka pale vipimo vitakapochukuliwa.


“Tupo kuhamasisha Upimaji wa Afya na utoaji wa Elimu kwa ujumla kuhusiana na afya. Mara zote tunasisitiza kufanya Kinga badala ya kusubiri kutibu. Kuna magonjwa Kama pressure, ni ugonjwa ambao hauonyeshi dalili yoyote lakini unaweza ukagundulika Mara baada ya kufika hospitalini”. Alisema Dkt. Tumaini.

Daktari Bingwa wa Magonjwa ya ndani, Dkt. Basla Tumaini


“Pia kwa akina mama kuanzia miaka 25 na kuendelea ni muhimu kupima Saratani ya kizazi. Ni vizuri Sana pale zinapotokea Fursa kama hizi wazitumie kupima Afya zao Kama saratasi ya Shingo ya kizazi na magonjwa mengine”. Aliongeza Dkt. Tumaini


Kwa Upande wake  Muumini wa kanisa Hilo, Bi. Rehema Simeon pamoja na Mkazi wa Tabata, Bw. Paschal Joshua walipongeza uendeshwaje wa zoezi hilo Huku wakiwataka Watanzania kutumia Fursa za Upimaji Afya Bure zinazotelewa na taasisi mbalimbali ili kujua Afya zao.


“Kwa ujumla Huduma ni nzuri na inasaidia Sana kwa watu tuliopo maeneo ya hapa Tabata kwani badala ya kwenda hospitali tunapimwa hapa Hapa, wananchi tu wajitokeze kwa wingi ili kujua Afya zao”Alisema Bw. Paschal Joshua.


“Nimefurahi kupata Vipimo kwasababu ukijua Afya yako unajua ni kitu gani kinakusumbua kwahiyo ninawashauri watu wote ambao mnataka kujua Afya zenu mje hapa Tabata au muende hosptalini ili mjue matatizo yanayosumbua Afya zenu na muweze kuyatibu”. Alisema Bi. Rehema Simeon.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »