BABU TALE AMKALIA KOONI WAZIRI AWESO

BABU TALE AMKALIA KOONI WAZIRI AWESO

NA MWANDISHI WETU-MOROGORO MBUNGE wa jimbo la Morogoro kusini mashariki Hamis Taletale(Babu Tale) amelazimika kupigia simu waziri wa maji Jumaa Aweso mbele ya wananchi baada ya kupokea maalalamiko kutoka kwa wananchi wa kijiji cha Kiroka juu ya gharama kubwa ya Maji. Hatua hiyo iekuja baada ya wananchi kulalaikia gaharaa ya unit moja kuuzwa kwa shilingo

NA MWANDISHI WETU-MOROGORO

MBUNGE wa jimbo la Morogoro kusini mashariki Hamis Taletale(Babu Tale) amelazimika kupigia simu waziri wa maji Jumaa Aweso mbele ya wananchi baada ya kupokea maalalamiko kutoka kwa wananchi wa kijiji cha Kiroka juu ya gharama kubwa ya Maji.

Hatua hiyo iekuja baada ya wananchi kulalaikia gaharaa ya unit moja kuuzwa kwa shilingo 1000 licha ya kuwa chanzo cha maji hayo ni Maporomoko ya mlima uruguru ambao upo kijijini hapo.

Amina saidi mmoja wa wanakijiji hao alisema kuwa walishangazwa na kauli za baadhi ya watendaji wa Ruwasa wilayani humo kuwa mita  zilizofungwa ni za kibiashara ambapo bei haiwezi kushika

“wametufungia mita wanatuambia ni za kibiashara kwa hiyo sisi ambao chanzo cha maji kipo hapa hapa tunauziwa shilingi 1000 kweli ni haki wakati tunajua maji ni huduma kwa wananchi iweje wao wafanye biashara?” alisea Amina

Naye diwani wa kata ya Kiroka Jamira taji alisema kuwa licha ya jitihada za viongozi wa kata hiyo katika kuomba bei hiyo kushuka ilishindikana kwa madai ya kusimamia sera ya maji.

Alisema hatua mbalimbali zinaendelea kuchukuliwa juu ya changamoto hiyo ambapo walikubaliana kuwepo na kikao cha pamoja kitakachojumuisha wananchi, Ruwasa na viongozi wa kata  ili kufikia muafaka

Akizunguza kwa njia ya simu Waziri Aweso ameahidi kufika kijijini hapo mara baada ya kumalizika vikao vya bunge la bajeti mwishoni wa mwezi wa sita mwaka huu ili kujionea uhalisia wa changamoto hiyo na kuipatia ufumbuzi.

“naomba ni waahidi wananchi wa Kiroka nitakuja mwenyewe kujionea hali ilivyo, niwahakikishie serikali ya awamu ya sita chini ya mama yetu Samia Suruhu Hassan ipo kwaajili ya kushughulikia matatizo ya wananchi na kuyamaliza kabisa” alisema

Kwa upande wake Babu Tale aliwataka wananchi kuendelea kuwa na subira wakati jambo hilo linafanyiwa kazi na serikali na kuwataka kuendelea na shughuli mbalimbali za kijamii ili kujiletea maendeleo.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »