EWURA yakabidhi mashuka katika vituo vya afya

EWURA yakabidhi mashuka katika vituo vya afya

Na Barnabas kisengi Dodoma  MAMLAKA ya udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji nchini (EWURA)imetoa msaada wa Mashuka 431 yenye thamani ya Shilingi Milioni tano kwa Vituo  vya Afya vya Makole,Hombolo,Mkonze na Kikombo kama sehemu ya kuadhimisha wiki ya utumishi wa Umma kwa lengo la kuboresha huduma za Afya kwa jamii. Akizungumza na Waandishi wa Habari

Na Barnabas kisengi Dodoma 

MAMLAKA ya udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji nchini (EWURA)imetoa msaada wa Mashuka 431 yenye thamani ya Shilingi Milioni tano kwa Vituo  vya Afya vya Makole,Hombolo,Mkonze na Kikombo kama sehemu ya kuadhimisha wiki ya utumishi wa Umma kwa lengo la kuboresha huduma za Afya kwa jamii.

Akizungumza na Waandishi wa Habari hii leo Jijini Dodoma mara baada ya kukabidhi msaada huo,Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa EWURA,Mhandisi Godfrey Chibulunje amesema kuwa kupitia wiki hilo la utumishi wa Umma wamekuwa wakirudisha huduma kwa jamii.

Hata hivyo Mamlaka hiyo katika wiki ya utumishi wa Umma iliweza kukutana na wafanyabiashara wa mafuta na kujua changamoto zao,malaka za maji kujua changamoto zao pamoja na kutoa mafunzo kwa watumishi wa mamlaka hiyo ili kuweza kutoa huduma bora katika sekta zote.

Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Jiji la Dodoma,DK.Andrew Method  ameishukuru EWURA  kwa msaaada huo  kwani inachochea ari ya uboreshaji wa utoaji huduma za Afya.

Katika hatua nyingine Dokta Method ametoa wito kwa wananchi kuendelea kuchukua tahadhari dhidi ya maambukizi ya virusi vya CORONA COVID19 kwa kunawa mikono na maji tiririka,kutumia vitakasa mikono pamoaj na kuvaa barakoa ikiwa ni pamoja na kuepuka mikusanyiko isiyo ya lazima.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Translate »