TAASISI ZA SANAA ZITUMIKE KUENDELEZA SANAA

TAASISI ZA SANAA ZITUMIKE KUENDELEZA SANAA

Na Mwandishi Wetu, Dar es salaam Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Hassan Abbasi amezisisitiza  Taasisi za Sanaa kutumika katika kuendeleza  sanaa na sio kuwa chombo cha kuonea na kukandamiza wasanii. Dkt. Abbasi amesema hayo  Juni 24, 2021 Jijini Dar  es Salaam alipomuwakilisha Waziri Mhe. Innocent Bashungwa kwenye Hafla ya Ufunguzi


Na Mwandishi Wetu, Dar es salaam


Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Hassan Abbasi amezisisitiza  Taasisi za Sanaa kutumika katika kuendeleza  sanaa na sio kuwa chombo cha kuonea na kukandamiza wasanii.


Dkt. Abbasi amesema hayo  Juni 24, 2021 Jijini Dar  es Salaam alipomuwakilisha Waziri Mhe. Innocent Bashungwa kwenye Hafla ya Ufunguzi wa Jukwaa la Elimu ya Masoko na Mabadiliko ya Matumizi ya Kidigitali kwa Kazi za Muziki Nchini (BOOMPLAY ARTISTE FORUM), iliyoandaliwa na Kampuni ya Transsnet MusicTanzania
“Taasisi zetu zinatakiwa ziwe sehemu ya kukuza Sanaa na si kugeuka kuwa Polisi ama Mgambo, tuzitangaze kazi za sanaa na tuwasaidie wasanii wetu kukua badala ya kuwakandamiza” amesema Dkt. Abbasi.


Ameongeza kuwa ni wakati sasa kwa  wasanii  kufanya kazi bora zaidi kwani jamii  imeikubali Sanaa, wasanii watumie vipaji vyao na ubunifu kufanya kazi bora na kujifunza namna ya kuuza kazi hizo kwa kutumia njia za kisasa kama Boomplay.


Dkt. Abbasi amesisitiza kuwa Serikali ipo tayari kushirikiana na wasanii kuboresha kazi zao na pia kuhakikisha wanapata namna tofauti za kuuza kazi zao kwa njia ya mtandao huku akiongeza kuwa imejipanga  kuboresha maslahi ya wasanii kama ilivyoahidiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, kuwa  mwisho wa mwaka huu itaanza kutoa mirabaha kwa wasanii.


Kwa upande wake Meneja Mkuu wa Kampuni ya Boomplay Tanzania, Natasha Stambuli amesema wako tayari kushirikiana na Serikali kukuza Sekta ya Sanaa nchini kwa kuwawezesha wasanii kuuza kazi zao kwa njia ya mtandao. 


Bi Natsha amesema kuwa Tanzania ina watumiaji milioni 11 hivyo kupitia kampuni  ya Boomplay wanaweza kufikisha kazi ya msanii kwa watu wengi zaidi na kwa kutumia njia za kisasa. 
Kongamano hilo limehudhuriwa na wasanii mbalimbali wa muziki na watayarishaji.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »