JAMII nchini imetakiwa kuitunza na kuielendeleza amani,kuwaombea dua, viongozi wa Taifa ili waweze kuongoza nchi kwa amani.

JAMII nchini imetakiwa kuitunza na kuielendeleza amani,kuwaombea dua, viongozi wa Taifa ili waweze kuongoza nchi kwa amani.

STATE HOUSE ZANZIBAR OFFICE OF THE PRESS SECRETARY PRESS RELEASE  Zanzibar                                                                                               25.06.2021 JAMII nchini imetakiwa kuitunza na kuielendeleza amani iliyopo na kuwaombea dua viongozi wa Taifa hili ili waweze kuongoza na kuiletea nchi maendeleo endelevu yenye kheri na tija. Akitoa neno la shukurani kwa niaba ya waumini wa Masjid Jamiu Zinjibar, Mazizini, Mkoa wa Mjini

STATE HOUSE ZANZIBAR

OFFICE OF THE PRESS SECRETARY

PRESS RELEASE

 Zanzibar                                                                                               25.06.2021

JAMII nchini imetakiwa kuitunza na kuielendeleza amani iliyopo na kuwaombea dua viongozi wa Taifa hili ili waweze kuongoza na kuiletea nchi maendeleo endelevu yenye kheri na tija.

Akitoa neno la shukurani kwa niaba ya waumini wa Masjid Jamiu Zinjibar, Mazizini, Mkoa wa Mjini Magharibi, mara baada ya sala ya Ijumaa Mkurugenzi wa msikiti huo Sheikh Shaaban Batwash alisema kuwa ni vyema kwa waumini na wananchi wote nchini wakawaunga mkono viongozi wao wa nchi katika kuiendeleza na kuisimamia amani.

msikiti wa Masjid Jamiu Zinjibar, Mazizini, Mkoa wa Mjini Magharibi visiwani Zanzibar.
Rais Alhaj Dkt. Hussein Mwinyi amejumuika pamoja na waumini wa msikiti wa Masjid Jamiu Zinjibar, Mazizini, Mkoa wa Mjini Magharibi katika sala ya ijuma.
Mkurugenzi wa msikiti wa Masjid Jamiu Zinjibar, Mazizini, Mkoa wa Mjini Magharibi, Sheikh Shaaban Batwash.
Rais Alhaj Dkt. Hussein Mwinyi amejumuika pamoja na waumini wa msikiti wa Masjid Jamiu Zinjibar, Mazizini, Mkoa wa Mjini Magharibi katika sala ya ijuma.
Rais Alhaj Dkt. Hussein Mwinyi amejumuika pamoja na waumini wa msikiti wa Masjid Jamiu Zinjibar, Mazizini, Mkoa wa Mjini Magharibi katika sala ya ijuma.

Katika sala hiyo ya Ijumaa ambapo Alhaj Dk. Hussein Mwinyi alijumuika pamoja na waumini wa msikiti huo, Mkurugenzi huyo wa Masjid Jamiu Zinjibar alisema kuwa uwepo wa amani ni amri ya Mwenyezi Mungu kwa viumbe wake hivyo, kuna kila sababu ya kuidumisha.

Alisisitiza haja ya kumuomba Mwenyezi Mungu kuzidisha amani iliyopo nchini na kueleza kuwa viongozi waliopo nchini wamekuwa wakifundisha na kuhimiza amani.

Aidha, alieleza kwamba jamii wana wajibu wa kuitunza amani na kuwaombea viongozi ili wawaongoze zaidi kwa hekima na busara huku wakimuombea dua Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan katika kutimiza siku zake mia za uongozi. Pia, alimuombea kwa Mwenyezi Mungu kumpa wepesi Rais wa Zanzibar na Menyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk. Hussein Mwinyi katika kuyatimiza yale yote yenye kheri na manufaa kwa wananchi wa Zanzibar.

Katibu wa Mufti wa Zanzibar Sheikh Khalid Ali Mfaume.

Akitoa hotuba ya sala ya Ijumaa msikitini hapo, Katibu wa Mufti wa Zanzibar Sheikh Khalid Ali Mfaume alisema kuwa kuwepo kwa amani kunapelekea kuimarika kwa uchumi.

Alisema kuwa mafungamano ya amani na uchumi ni makubwa sana kwani maendeleo hayawezi kupatikana kama hakuna amani hivyo, ni vyema kuiendeleza na kuitunza neema hiyo ili isije ikaondoka.

Alisema kuwa amani, usalama na utulivu ni maisha ya viumbe vyote walioumbwa na Mwenyezi Mungu wakiwemo binaadamu na hata wanyama nao pia, huhitaji amani.

Hivyo, Sheikh Khalid Ali Mfaume alisema kuwa kiongozi mzuri ni yule anayehimiza amani, umoja na mshikamano kwa wale anao waongoza.

“Tusizungumze amani kila siku bali tuzungumze amani kila dakika kwani amani ndio maisha yetu, amani ndio maendeleo yetu, amani ndio mustakabali wetu kwani huwezi kulima, kusoma bila ya kuwepo kwa amani….basi kwa msingi huo asitokee mtu akaiharibu amani kwani ataharibu amani….mshairi anasema uhifadhi ulimi wako mwanaadamu kwa sababu ulimi ni nyoka mwenye sumu sana…kunyamaza ni salama…kwani sio kila kitu unasema”, alisisitiza Sheikh Khalid.

Aidha, Khalid pia, aliitaka jamii kushirikiana katika kupiga vita matumizi ya dawa za kulevya pamoja na aina zote za vilevi kwani matumizi yake hupelekea kuondoka kwa amani hasa kwa vijana.

Alieleza kwamba iwapo vijana watajihusisha na matumizi ya dawa za kulevya watapelekea kudhorotesha uchumi pamoja na amani iliyopo kuanzia ngazi ya familia, jamii hadi Taifa. Sambamba na hayo, Sheikh Khalid aliitumia fursa hiyo kueleza kwamba matumizi ya dawa za kulevya na vilevi vyengine huharibu uchumi kwani baadhi ya watumiaji huingia kwenye wizi ambapo hivi sasa hali hiyo imejitokeza hata vijijini ambapo kumeibuka wizi wa mifugo na mazao.

Wakati huo huo, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk. Hussein Ali Mwinyi alifika nyumbani kwa mwanasiasa mkongwe na Muasisi wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Bi Asha Simba Makwega huko nyumbani kwake Kilimani, Wilaya ya Mjini Mkoa wa Mjini Magharibi kwa ajili ya kumsalimia na kumjuulia hali.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk. Hussein Ali Mwinyi akiwa nyumbani kwa mwanasiasa mkongwe na Muasisi wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Bi Asha Simba Makwega Kilimani, Wilaya ya Mjini Mkoa wa Mjini Magharibi kwa ajili ya kumsalimia na kumjuulia hali.

Mapema asubuhi, Alhaj Dk. Mwinyi alijumuika na ndugu, jamaa, marafiki pamoja na wananchi mbali mbali katika sala ya kumsalia Marehemu Mzee Msuri Muhidini huko katika msikiti wa Muembe mimba, Wilaya ya Mjini Mkoa wa Mjini Magharibi.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk. Hussein Ali Mwinyi amejumuika na ndugu, jamaa, marafiki pamoja na wananchi mbali mbali katika sala ya kumsalia Marehemu Mzee Msuri Muhidini katika msikiti wa Muembe mimba, Wilaya ya Mjini Mkoa wa Mjini Magharibi.

Alhaj Dk. Mwinyi aliwaomba wana familia kuwa na subira katika kipindi hichi kigumu cha msiba wa mzee wao Marehemu Mzee Msuri Muhidini ambaye ameacha kizuka mmoja na watoto wanne na kumuombea kwa Mwenyezi Mungu ailaze roho yake marehemu mahala pema peponi, Amin.

Hadi anafariki dunia Marehemu Mzee Msuri Muhidini alikuwa Mjumbe wa Kamati ya Siasa Mkoa wa Mjini ambaye pia, aliwahi kuwa Mwenyekiti wa Tawi la Mikunguni, Jimbo la Kwahani katika Mkoa wa Mjini Magharibi.

Rajab Mkasaba, Ikulu Zanzibar

Postal Address: 2422 Tel.:0777427449. Fax: 024 2231822 

 E-mail: rajabmkasaba@yahoo.co.uk

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »