Watumishi wa Afya wametakiwa kuwa mabalozi wazuri wanapotoa huduma za afya .

Watumishi wa Afya  wametakiwa kuwa mabalozi wazuri wanapotoa huduma za afya .

WATUMISHI wa Afya wa kada mbalimbali wametakiwa kuwa mabalozi wazuri katika utoaji huduma za afya kwakufuata misingi ya haki za binadamu na utawala bora katika utoaji wa huduma za afya ili kuweza kuondoa kero na malalamiko miongoni mwa jamii katika sekta ya afya. Kauli hiyo imetolewa leo Jijini Dodoma na Mkuu wa Wilaya ya Dodoma

WATUMISHI wa Afya wa kada mbalimbali wametakiwa kuwa mabalozi wazuri katika utoaji huduma za afya kwakufuata misingi ya haki za binadamu na utawala bora katika utoaji wa huduma za afya ili kuweza kuondoa kero na malalamiko miongoni mwa jamii katika sekta ya afya.

Kauli hiyo imetolewa leo Jijini Dodoma na Mkuu wa Wilaya ya Dodoma mjini Jabir Shekimweli kwaniaba ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma,Anthony Mtaka wakati akifungua mafunzo kuhusu haki za binadamu na utawala bora kwa watumishi wa afya wa Hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Dodoma ambayo yameratibiwa na Tume ya Haki za binadamu na utawala bora nchini.

Amesema kuwa kupitia mafunzo hayo  wataenda kuwa chachu katika utendaji wao na hivyo kuweza Kukaa na kuangalia kiwango gani walichonacho juu ya haki za binadamu na misingi ya utawala bora.

Hata hivyo ameitaka Tume hiyo kuhakikisha inaweka utaraibu wa kutoa mafunzo katika sekta hiyo kwa lengo la kuwajengea uwezo.

Awali akitoa taarifa kuhusiana na mafunzo hayo Kamishina wa Tume ya Haki za Binadamu na utawala bora nchini,Dokta Fatma Rashid Khalfan  amesema kuwa lengo la mafunzo hayo yanayohusu Haki za Binadamu na Utawala bora ni kuwawezesha watumishi wa Sekta hiyo kuyatambua,kuyajua na kuishi katika misingi ya utawala bora na kutambua mchango wa sekta ya afya.

Naye Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Dodoma,Dk Ernest Ibenzi ameishukuru Tume kwa mafunzo hayo huku akiahidi kuendelea kutoa huduma za afya kwa weledi mkubwa na kufuata misingi ya haki za binadamu na utawala bora.

Mafunzo hayo ya siku tatu yanatolewa kwa jumla ya watumishi 75 wa Hospitali hiyo ya rufaa ya Mkoa wa Dodoma ambapo pia yanafanyika Nchini kote ikiwemo Zanzibar kwa watumishi wote wa Sekta ya Afya.

Na Barnabas kisengi Dodoma June 25  2021.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »