Diwani Kata ya Sandali Manispaa ya Temeke Mhe. Christopher Kabalika awasilisha utelekezaji wa Ilani ya CCM mbele ya Halmashauri Kuu

Diwani Kata ya Sandali Manispaa ya Temeke Mhe. Christopher Kabalika awasilisha utelekezaji wa Ilani ya CCM mbele ya Halmashauri Kuu

Diwani wa Kata ya Sandali Manispaa Temeke Mhe. Christopher Kabalika amesoma taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi CCM ya mwaka 2020-2025 mbele ya Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi ngazi ya Kata hiyo ikiwa imetimia miezi sita tangu aapishwe kuwa Diwani wa Kata hiyo. Katika taarifa yake, Mhe. Kabalika ameeleza jinsi alivyotekeleza


Diwani wa Kata ya Sandali Manispaa Temeke Mhe. Christopher Kabalika amesoma taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi CCM ya mwaka 2020-2025 mbele ya Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi ngazi ya Kata hiyo ikiwa imetimia miezi sita tangu aapishwe kuwa Diwani wa Kata hiyo.

Katika taarifa yake, Mhe. Kabalika ameeleza jinsi alivyotekeleza mambo kadha wa kadha yaliyoelekezwa kwenye ilani ya CCM ya mwaka 2020-2025 kama vile kusikilizq na kutatua kero za wananchi, kusimamia uadilifu, utawala bora, wajibikaji, vita dhidi ya rushwa, kuimamia utekelezaji wa miradi ya maendeleo, kuimarisha ulinzi na usalama.



Mambo mengine ni upatikanaji wa huduma bora za jamii kama, Afya, Elimu, Maji na miundo mbinu.

Katika kutekeleza hayo, Mhe. Kabalika amesema kamati ya Maendeleo ya Kata iliyoko chini yake wamegusa kila idara kuhakikisha wanawatumikia wananchi ipasavyo.

Katika uwakilishi, Mhe. Kabilika amesema kuwa amehudhuria vikao vyote vya kisheria ndani ya Manispaa ya Temeke pamoja na Semina mbalimbali kujipatia maarifa na ujuzi wa kutekeleza majukumu yake.




Kwa upekee Diwani Mhe. Kabalika ametaja baadhi ya miradi ya maendeleo aliyoyatekeleza ikiwa ni pamoja na ; ujenzi wa mfereji wa mpogo ambao ulikuwa kero kwa jamii kwa miaka kadhaa kwa kutoa harufu chafu, pili Mhe. Kabalika amefanya ukarabati katika baadhi ya barabara kwa kuweka taa za barabarani, kuweka alama za pundumili kwenye maeneo ya kuvukia waenda kwa miguu hasa wanafunzi pamoja na ujenzi wa daraja kwa kushirikiana na Wakala wa Barabara mijini na Vijijini (TARURA).



Kwa upande wa sekta ya Elimu, Mhe. Kabalika amesema kuwa wamefanikiwa kufanikisha Sera ya Elimu kuanzia Darsa la kwanza hadi Kidato cha Nne, pia wamekarabati na kujenga baadhi ya miundo mbinu katika shule za msingi na sekondari ndani ya Kata ya ya Sandali ikiwemo, ujenzi wa Madarasa, tundu za vyoo 11, utengenezaji wa madawati 200 na viti 200.

Katika sekta ya Afya, Mhe. Diwani ameeleza mafanikio makubwa ikiwa ni pamoja kuleta huduma ya Ultra Sound katika Zahanati ya Kata ya Sandali pamoja na ujenzi vyumba vitatu katika zahanati hiyo.

Aidha Mhe. Kabalika amesema kuwa katika huduma za kijamii juhudi kubwa zimefanyika kuhakikisha wananchi wananufaika na fursa zinazototewa na kujikwamua kiuchumi ikiwa ni pamoja na kusajili vikundi 39, ambapo Mhe. Diwani Kabalika amekuwa mstari wa mbele kuwasaidia kwa kuchangia zaidi ya Tsh. 2, 000, 000/= katika usajili na kufungua akaunti za vikundi.


Pamoja na mafanikio hayo makubwa katika utekelezaji wa Ilani ya CCM ya Mwaka 2021-2021, Mhe. Diwani Kabalika amesema ndani ya kata hiyo bado kuna changamoto kwenye sekta ya ulinzi na usalama kutokana na uwepo matukio ya ukabaji, uporaji wa kutumia pikipiki. Katika kudhibiti na kukabiliana na matukio hayo, Ofisi ya Diwani huyo imeweza kukarabati kituo kidogo cha Polisi kilichopo mtaa wa Mkwinda pamoja na kutoa Elimu ya ulinzia shirikishi kwa ngazi zote.



Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Kata ya Sandali, walipokea kwa shangwe na kuunga hoja taarifa hiyo ya utekelezaji wa Ilani ya CCM ya Mwaka 2020-2021 iliyowasilishwa kwao na Diwani wa Kata hiyo, Mhe. Christopher Kabalika.




Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »