WAZIRI MCHENGERWA AZINDUA MFUMO RASMI WA KUSIKILIZA KERO ZA WATUMISHI WA UMMA

WAZIRI MCHENGERWA AZINDUA MFUMO RASMI WA KUSIKILIZA KERO ZA WATUMISHI WA UMMA

Na Barnabas Kisengi Dodoma Kutokana na changamoto ya wafanyakazi wa utumishi wa umma na wananchi kuwa na malalamiko na kero mbalimbali zinazowakuta katika utendaji  wa kazi mbalimbali za utumishi wa umma imepelekea Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora kuzindua mfumo wa sema na Waziri wa Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora ili watumishi

Na Barnabas Kisengi Dodoma


Kutokana na changamoto ya wafanyakazi wa utumishi wa umma na wananchi kuwa na malalamiko na kero mbalimbali zinazowakuta katika utendaji  wa kazi mbalimbali za utumishi wa umma imepelekea Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora kuzindua mfumo wa sema na Waziri wa Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora ili watumishi waweze kusikilizwa kero na changamoto kwa wakati kwa kutumia mfumo huu ambao waziri atakuwa akifahamu kwa wakati. 


Awali akiongea na watumishi wa Wizara hiyo na waandishi wa habari, Waziri wa Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora Mohammed Mchengrwa  Amesema watumishi wamekuwa na malalamiko mengi na muda mrefu ambayo yamekuwa yayatatuliwi kwa wakati hivyo mfumo huu utakuwa chachu kwao kwakuwa watakuwa wanawasiliana na Mimi na wasaidizi wangu wa ofisini moja kwa moja na kupata majibu yao kwa wakati.


“kumekuwa na malalamiko mengi nikiwa napigiwa simu hasa upandishaji wa vyeo,madaraka na mishahara kwa watumishi wengi sasa natoa maagizo kwa afisa utumishi ambaye amefanya makusudi kutompandisha mtumishi daraja kwa makusudi hatuta mwachwa afisa utumishi huyo salama tutamchukulia hatua za kinidhamu kwakuwa hajamtendea haki mtumishi huyo”amesema Mohammed Mchengrwa.


Waziri Mchengerwa amesema hivi karibuni wamewapandisha madaraja watumishi 76 elfu kati ya watumishi elfu 91 na zoezi hilo linaendelea kadri ya bajeti inavyo patikana na amewasisitiza maafisa utumishi katika maeneo yao kuhakikisha watumishi wenye sifa wanapandishwa madaraja na kuacha kabisa urasimu wa kuwaonea watumishi wenye sifa za kupandishwa daraja kwakuwa serikali ya awamu ya sita itafuatilia kwa makini.


Awali akimkaribisha waziri Naibu Waziri wa Ofisini ya Rais Utumishi na Utawala Bora Deogratus Ndejembi  amesema mfumo huo wa sema usikike na waziri utakuwa umetoa fursa kubwa kwa watumishi wa umma kwa kutoa malalamiko, maomi, mapendekezo na pongezi katika serikali ya awamu ya tano na hata watumishi walio ndani vijijini ambako Kuna shida ya kimtandao na wasio tumia simu njanja bado watakuwa na nafasi ya kuweze kutumia simu ya kawaida kwa kutuma ujumbe wa msg za kawaida kwa kutumia simu zao kwa  msg kwa kuweka nyota 152 nyota 00 reli kisha utakwenda namba tisa na kufuata maelekezo


“Mfumo huu uliozinduliwa leo utatusaidia Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora kufahamu moja kwa mojo changamoto za watumishi na wananchi kwa ujumla ambao watakuwa na malalamiko mbalimbali na maoni katika ofisi mbalimbali na sisi wasaidizi wa Mhe. Rais tutafahamu mkoa wilaya ofisi kwenye changamoto na itatusaidi kufahamu mambo mbalimbali katika katika wizara yetu na kuweza kuwajibu watumishi na wananchi mambo mbalimbali watakayokuwa wameuliza na mfumu juu utakuwa unapokea malalamiko,maoni,mapendekezo na pongezi kutoka kwa watumishi na wananchi mbalimbali hapa nchi”amesema Ndejembi

1 comment
Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

1 Comment

  • Sylvanus Rwechungula
    June 30, 2021, 4:31 am

    Pole na majukumu yako mh! Natoka Dodoma jiji,pongezi kwa kupandisha madaraja baadhi ya watumishi.Je ambao tumesalia hadi lini? Mf Mimi nimeajiliwa 2014 Hadi sasa japo nimepata barua juzi ya kupanda,mshahara nimekuta uleule.

    REPLY

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »