WAISLAMU WATAKIWA KUZISAIDIA TAASISI ZA KIDINI KUTATUA CHANGAMOTO

WAISLAMU WATAKIWA KUZISAIDIA TAASISI ZA KIDINI KUTATUA CHANGAMOTO

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Al-haji Dk. Hussein Ali Mwinyi amewataka waislamu Nchini kujitolea kwa hali na mali kuzisaidia taasisi za dini ya Uislamu ili kutatua changamoto zinazozikabili taasisi tofauti. Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Hemed Suleiman Abdulla alieleza hayo wakati akimuakilisha Rais Dk. Hussein Ali Mwinyi katika kilele

Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Sharifa Omar Khalfan akiwa pamoja na waumini waliohudhuria katika kilele cha sherehe za Tanzania Muslim teachers Association Day  zilizofanyika katika viwanja vya Madrasat Shamsiya ilipo Tanga.
Waumini wa Dini ya Kislamu kutoka Mikoa mbali mbali ya Tanzania wakimskiliza kwa Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla katika kilele cha sherehe za Tanzania Muslim teachers Association Day  zilizofanyika katika viwanja vya Madrasat Shamsiya ilipo Tanga.
Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Abubakari Zubeir Ally akiwasisitiza waislamu waliohudhuria katika kilele cha sherehe za Tanzania Muslim teachers Association Day  zilizofanyika katika viwanja vya Madrasat Shamsiya ilipo Tanga kuendelea kuchukua Tahadhari dhidi ya Maradhi ya Covid-19.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla akiwakumbusha Waumini kujitokeza kuchangia kutatua changamoto zinazozikabili taasisi za Kidini ili kutoa fursa ya kuwajenga vijana katika maadili mema.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Al-haji Dk. Hussein Ali Mwinyi amewataka waislamu Nchini kujitolea kwa hali na mali kuzisaidia taasisi za dini ya Uislamu ili kutatua changamoto zinazozikabili taasisi tofauti.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Hemed Suleiman Abdulla alieleza hayo wakati akimuakilisha Rais Dk. Hussein Ali Mwinyi katika kilele cha sherehe za Tanzania Muslim teachers Association Day  zilizofanyika katika viwanja vya Madrasat Shamsiya ilipo Tanga.

Alieleza kuwa, kutatua changamoto zinazozikabili Taasisi zinazozimamia dini ya waislam sio jukumu la mtu mmoja mmoja bali lina hitaji nguvu za pamoja na mashirikino miongoni mwa waislam kwa lengo la kuwajengea vijna mustakbali mwema wa maisha yao ya baadae.

Makamu wa Pili wa Rais alisema viongozi wa Taasisi ya Tanzania Muslim teachers Association tayari imeonesha njia katika kuwafinyanga vijana wa kislamu kutoka maeneo mbali mbali ya Tanzania kwa kuwapatia elimu yenye manufaa hapa duniani na kesho akhera hivyo ni jambo la busara waislamu kujitokeza kuunga mkono jitihada hizo.

Alifafanua kwamba, Juhudi hizo za walimu zimeweza kuzaa matunda kutokana na vijana wa madrasa kuwa na uwezo mzuri wa kufafanua masuala mbalimbali yanayoshikamana na dini ya uislamu.

“Nimefurahi sana kusikia masuala mbali mbali yakifafanuliwa na vijana wetu wa Madrasat Shamsiya” Alisema Mhe. Hemed

Akibainisha changamoto zinazowakabili walimu  hao Makamu wa Pili wa Rais alisema  uhaba wa gharama za uwendeshaji  hivyo aliwasisitiza waisilam kukaa pamoja na kupendekeza njia za kutatua changamoto hiyo.

“Changamoto ya miundo mbinu isiyojitosheleza kama vile Mabweni,vitanda,maktaba,matibabu na nyenginezo nimezisikia,na nitaziwasilisha kwa Mhe Dk. Hussen Ali Mwinyi ili kwa pamoja tuone namna tutakavyo weza kusaidi kutatua baadhi ya changamoto hizo”Alifafanua Makamu wa Pili  wa Rais

Sambamba na hayo, aliwaomba viongozi pamoja na waumini walio hudhuria kuendelea kudumisha Amani na mshikamano baina ya Waislam na Watanzania kwa ujumla kwa kuwaombea dua viongonzi wakuu wa Nchi akiwemo Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan na Rais wa Zanzibar  na mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hssen Ali Mwinyi ili waendelee kuongoza vyema.

Nae, Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Abubakari Zubeir Ally  aliwakumbusha waumini waliohudhuria katika kilele cha sherehe hizo kuenzi na kuendelea kumuombea Dua muasisi wa Taasisi hiyo Almarhumu Sheikh Mohamed Ayyub kutokana na jambo jema aliloliasisi akishirikiana na wenzake jambo ambalo limesaidia kuhuwisha imani za waumini.

Sheikh Abubakar Zubeir aliwakubusha waumini kuendelea kuchukua tahadhari pamoja na kufuata maelekezo yanayotolewa na wataalamu wa Afya juu ya kujikinga na maradhi ya Covid- 19 ambayo yamekuwa tishio ulimwenguni kote.

Mapema Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alipokea Maandamano ya Amani yaliowashirikisha waumini kutoka Mikoa mbali mbali ya Tanzania.

Tanzania Muslim Teachers Association (TAMTA) imetimiza miaka Sitini na nne (64) Tangu ilipoanzishwa Mnamo mwaka 1957.

…………………………….

Kassim Abdi

Ofisi ya Mkamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar.

01/07/2021.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »