Wachungaji wapewa maelekezo kuhusu Corona.

Wachungaji wapewa maelekezo kuhusu Corona.

ASKOFU wa Kanisa la Calvary Assemblies of God (CAG) jimbo la Kagera, Damian Rwabutikula amewataka wachungaji mkoani humo kuzingatia masharti na maelekezo ya wataalamu wa afya katika utendaji wao wa kutoa huduma za kichungaji kwa waumi wao jinsi ya kujikinga na ugonjwa wa Corona. Askofu Rwabutikula ametoa wito huo katika ibada ya kuwasimika wachungaji wa

ASKOFU wa Kanisa la Calvary Assemblies of God (CAG) jimbo la Kagera, Damian Rwabutikula.
ibada ya kuwasimika wachungaji wa kanisa hilo.
ibada ya kuwasimika wachungaji wa kanisa hilo
ibada ya kuwasimika wachungaji wa kanisa hilo
Katibu Msaidizi wa Kanda ya Mashariki (C.A.G), Askofu Amos Peter kutoka jijini Dar es Salaam

ASKOFU wa Kanisa la Calvary Assemblies of God (CAG) jimbo la Kagera, Damian Rwabutikula amewataka wachungaji mkoani humo kuzingatia masharti na maelekezo ya wataalamu wa afya katika utendaji wao wa kutoa huduma za kichungaji kwa waumi wao jinsi ya kujikinga na ugonjwa wa Corona.

Askofu Rwabutikula ametoa wito huo katika ibada ya kuwasimika wachungaji wa kanisa hilo waliomaliza elimu ya diploma na viongozi wa vijana wa jimbo hilo, ibada iliyofanyika katika Kanisa la Chonyonyo lililopo wilayani Karagwe mkoani Kagera.

Amesema wachungaji hao wanatakiwa kupeleka elimu sahihi kwa waumini wao, wawaelimishe na kuwaelekeza jinsi ya kujikinga na Corona kwani ugonjwa huu upo na unaua, wawafundishe umuhimu wa kuvaa barakoa na kuweka vibuyu chirizi vyenye maji tiririka pamoja na sabuni na kunawa mikoni mara kwa mara ili kujikinga na ugonjwa huo.

Naye Katibu Msaidizi wa Kanda ya Mashariki (C.A.G), Askofu Amos Peter kutoka jijini Dar es Salaam amewaonya wachungaji kuacha tabia ya kushabikia kitu chochote kinachoipinga serikali kwani itawapunguzia hali ya kuaminiwa na serikali na jamii kwa ujumla.

Amesema wachungaji ni watu wa kuaminiwa tangu enzi, ni kioo cha jamii na ili waaminiwe na kuheshimiwa na wanaowaongoza inatakiwa kutengeneza imani kwa serikali ili taifa linapohitaji majibu liyapate kutoka kwao.

Na Nyemo Malecela – Kagera.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »