SOMO LA LEO: Yeremia 29:11.

SOMO LA LEO: Yeremia 29:11.

Kuna siku nilipeleka koti langu la suti kwa fundi cherehani anirekebishie mfuko ulikuwa umefumuka.Mara jamaa akageuza koti kwa ndani na kisha akaanza kulifumua fumua badala ya kuushona mfuko wenyewe!!!Nikahamaki nikamwambia, “Mzee unapaswa kushona, sio kufumua halafu nina haraka ujue. Mbona ni kazi rahisi tu ya faster.” Lakini yeye alijibu tu, “NAJUA”. Hilo jibu lilinigusa na sikuweza

Kuna siku nilipeleka koti langu la suti kwa fundi cherehani anirekebishie mfuko ulikuwa umefumuka.
Mara jamaa akageuza koti kwa ndani na kisha akaanza kulifumua fumua badala ya kuushona mfuko wenyewe!!!
Nikahamaki nikamwambia, “Mzee unapaswa kushona, sio kufumua halafu nina haraka ujue. Mbona ni kazi rahisi tu ya faster.” Lakini yeye alijibu tu, “NAJUA”. 
Hilo jibu lilinigusa na sikuweza kuzungumza tena. Yeye ni fundi cherehani, na mimi ni mteja tu. Na kweli mwisho wa siku mfuko ulirekebishika na nikafurahi nikamwambia ASANTE fundi.
Kuna vile tunapeleka mahitaji yetu kwa MUNGU halafu mambo yanakwenda tofauti na matarajio yetu.
🪡 Yani unamwambia Baba angalia biashara yangu imeyumba… MUNGU anajibu, ‘NAJUA’. 
🪡 Baba, mchumba wangu ameniacha … MUNGU anajibu, ‘NAJUA’. 
🪡 Sina pesa ya kulipia kodi yangu… MUNGU anajibu, ‘NAJUA’ 
🪡 Baba angalia … nimepoteza kazi yangu na nina familia inanitazama …. “NAJUA” 
🪡 Baba niko kwenye ndoa kwa miaka na sina mtoto …. “NAJUA” 
Mara nyingi wakati BWANA anatutengeneza, Anaanza kwa ‘kutufumua’. Kuna vile anavuruga kabisa kujiamini kwetu, falsafa zetu zote, kiburi chetu na unyenyekevu wetu bandia. 
Ni tabia ya MUNGU kufumua vitu na kuunda kulingana na mapenzi yake mema. 
Kwa kweli, MUNGU habagui mtu, Yeye hufanya apendavyo. Kuna mambo yanatutoa MACHOZI lakini hayamzuii kuchana maisha yetu akiwa kazini. Sisi tunaangalia kuanzia kwa nje, Yeye anaanzia kushughulikia ndani. 
MUNGU ANAJUA UTAFURAHIA MATOKEO ya KAZI YAKE! Anajua una hitaji nini hasa hata kabla ya kuomba. Ndio maana tunapolalamika, Anajibu hivi: ‘NAJUA’. 
🍍 Yeremia 29:11″Kwa maana NAJUA mawazo ninayowawazia ninyi, asema BWANA, mawazo ya amani, wala si ya mabaya, kuwapa ninyi tumaini siku zenu za mwisho.”*#Mungu Atubariki*

Na. Mwalimu Babu Musa Abraham KAMBAGHA.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »