Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, amesema kuwa wakati mwingine dini na siasa vinaendana lakini pia wakati mwingine ni vitu vivyokinzana ambapo amesisitiza kwamba vyote hivyo vinatakiwa kutazamwa kwa umakini. Rais Samia ametoa kauli hiyo leo Julai 8, 2021, mkoani Morogoro aliposhiriki Mkutano Mkuu wa Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT),
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, amesema kuwa wakati mwingine dini na siasa vinaendana lakini pia wakati mwingine ni vitu vivyokinzana ambapo amesisitiza kwamba vyote hivyo vinatakiwa kutazamwa kwa umakini.
Rais Samia ametoa kauli hiyo leo Julai 8, 2021, mkoani Morogoro aliposhiriki Mkutano Mkuu wa Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT), ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya siku mbili mkoani humo aliyoianza hapo jana akitokea Jijini Dodoma.
Rais Samia pia amezitaka taasisi za kidini zinazotoa huduma ya kielimu na afya kuweka uwazi katika utendaji wa kazi zao ikiwemo ukaguzi wa hesabu ili kutoa fulsa kwa maafisa wanaotoza kodi kuweka utaratibu mzuri.
Kwa upande wake mwenyekiti wa jumuiya ya kikristo Tanzania Askofu Dkt Alinisa Cheyo amesema kuwa pamoja na mambo mengine makanisa yanakabiliwa na changamoto ya upatikanaji wa vibali vya kazi hasa kwa raia wa kigeni ambao wanakuja kutoa huduma katika taasisi za afya na elimu.
Leave a Comment
Your email address will not be published. Required fields are marked with *