RAIS DKT. MWINYI APONGEZA TAMASHA LA ZIFF KATIKA KUTANGAZA UTALII NA URITHI WA ZANZIBAR

RAIS DKT. MWINYI APONGEZA TAMASHA LA ZIFF KATIKA KUTANGAZA UTALII NA URITHI WA ZANZIBAR

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi amesema kuwa kuwepo kwa Tamasha la Kimataifa la Filamu la Zanzibar (ZIFF), ni njia moja wapo ya kuukuza na kuutangaza utalii pamoja na urithi wa Zanzibar. Rais Dk. Mwinyi aliyasema hayo leo Ikulu Jijini Zanzibar wakati alipokutana na kufanya mazungumzo na uongozi

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi amesema kuwa kuwepo kwa Tamasha la Kimataifa la Filamu la Zanzibar (ZIFF), ni njia moja wapo ya kuukuza na kuutangaza utalii pamoja na urithi wa Zanzibar.

Rais Dk. Mwinyi aliyasema hayo leo Ikulu Jijini Zanzibar wakati alipokutana na kufanya mazungumzo na uongozi wa Tamasha la Kimataifa la Filamu la Zanzibar (ZIFF), ukiongozwa na Mkurugenzi wake Profesa Martin Muhando.

Katika maelezo yake, Rais Dk. Mwinyi alisema kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ina unga mkono juhudi hizo zinazochukuliwa na ZIFF ambazo alisisitiza kwamba ndio njia muhimu ya kuukuza na kuutangaza utalii wa Zanzibar.

Rais Dk. Mwinyi alitumia fursa hiyo kutoa pongezi kwa uongozi huo wa ZIFF kwa kazi kubwa inayofanya ambayo imekuwa ikileta tija katika kuutangaza na kuukuza utalii visiwani Zanzibar kwa kila mwaka.Alisisitiza kwamba Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Awamu ya Nane itaendelea kutoa ushirikiano wake katika kuhakikisha Tamasha hilo linaendelea kupata mafanikio zaidi.Akieleza kuhusu suala zima la uigizaji wa Filamu kwa vijana, Rais Dk. Mwinyi alisema kuwa ni vyema vijana wakapewa elimu sambamba na kuunganishwa pamoja ili waweze kukuza na kuendeleza vipaji vyao walivyonavyo katika tasnia mbali mbali.

Rasi Dk. Mwinyi alisema kuwa ni vyema ikawepo sehemu maalum ya kutoa vipaji hasa ikizingatiwa kwamba vipaji hapa Zanzibar vipo na kinachohitajika hivi sasa ni kuendelezwa tu na kutoa shukurani kwa ZIFF kwa kuendeleza Tamasha hilo.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »