BENKI KUU YATANGAZA KUONGEZA KASI YA MIKOPO SEKTA BINAFSI

BENKI KUU YATANGAZA KUONGEZA KASI YA MIKOPO SEKTA BINAFSI

Na Barnabas Kisengi,Dodoma , GAVANA wa Benki  Kuu ya Tanzania (BOT)Profesa Florens Luoga amesema kuwa Benki hiyo,imechukua hatua mbalimbali ambazo zinalenga kuongeza kasi ya mikopo kwenda sekta binafsi ikiwa ni pamoja na kupunguza riba hadi kufikia asilimia 9 ili wawekezaji wa ndani waweze kukopa na kuikwamua sekta ya kilimo. Sanjari na hilo amesema hatua  nyingine ni pamoja

Na Barnabas Kisengi,Dodoma

,

GAVANA wa Benki  Kuu ya Tanzania (BOT)Profesa Florens Luoga amesema kuwa Benki hiyo,imechukua hatua mbalimbali ambazo zinalenga kuongeza kasi ya mikopo kwenda sekta binafsi ikiwa ni pamoja na kupunguza riba hadi kufikia asilimia 9 ili wawekezaji wa ndani waweze kukopa na kuikwamua sekta ya kilimo.

Sanjari na hilo amesema hatua  nyingine ni pamoja na kuanzishwa kwa Mfuko maalum wenye thamani ya Shilingi Trilioni 1kwaajili ya kukopesha mabenki na Taasisi za fedha kwa asilimia 3 ambazo nazo zitatakiwa kutoza riba isyozidi asilimia10.

Gavana Luoga ametoa Kauli hiyo  leo Jijini Dodoma wakati  akizungumza na waandishi wa Habari kuhusiana na hatua za kisera ambazo Benki kuu imechukua ili kuongeza upatikanaji wa mikopo kwa sekta binafsi na kupunguza viwango vya riba.

Aidha amebainisha kuwa hatua hizo za kisera ambazo zimechukuliwa na Beki kuu ni kwa mujibu wa Sura namba 197 na sheria ya mifumo ya Malipo ya Taifa sura ya 437.

Katika hatua nyingine benki kuu imeziagiza benki za biashara na Taasisi za Fedha kuweka na kutekeleza mikakati ya kupunguza Riba za mikopo na kuhamasisha upatikanaji wa amana

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Translate »