RAIS DKT. MWINYI AMEKABIDHIWA TUZO NA RAIS WA UFARANSA

RAIS DKT. MWINYI AMEKABIDHIWA TUZO NA RAIS WA UFARANSA

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi ametunukiwa Tuzo ya Juu ya Heshima inayofahamika kama “Legion d’ Honner” na Rais wa Jamhuri ya Ufaransa Emmanuel Macron kutokana na mchango wake mkubwa wakati akiwa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa la Tanzania. Rais Dk. Mwinyi alitunukiwa Tuzo hiyo leo

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi ametunukiwa Tuzo ya Juu ya Heshima inayofahamika kama “Legion d’ Honner” na Rais wa Jamhuri ya Ufaransa Emmanuel Macron kutokana na mchango wake mkubwa wakati akiwa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa la Tanzania.
 
Rais Dk. Mwinyi alitunukiwa Tuzo hiyo leo na Balozi wa Ufaransa Nchini Tanzania Mhe. Frederic Clavier kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Ufaransa Emmanuel Macron, tukio lililofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar ambapo Balozi huyo alihudhuria akiwa na ujumbe wake.
 
Rais Dk. Mwinyi alitoa shukurani zake za dhati kwa Rais wa Ufaransa  Emmanuel Macron kwa kumtunukia Tuzo hiyo iliyotokana na kuthamini kwa dhati mchango wake  mkubwa alioutoa wakati akiwa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa la Tanzania takriban kwa miaka 10.
 
Katika maelezo yake  Rais Dk. Mwinyi alisema kuwa amepokea Tuzo hiyo ambayo ni heshima kubwa kwani hutolewa kwa  watu mbali mbali duniani hasa kwa mchango wake unaopaswa kupewa heshima hiyo.
 
Rais Dk. Mwinyi alieleza kwamba takriban miaka 10 akiwa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa la Tanzania ambapo katika kipindi hicho Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeweza kusaidia kwa kiasi kikubwa katika operesheni  tano za kudumisha amani hasa zile za Bara la Afrika ambazo zote zimeonesha mafanikio makubwa.
 
Hivyo, Rais Dk. Mwinyi alitoa shukurani kwa heshima hiyo na kueleza kwamba, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itaendelea kushirikiana na Jamhuri ya Ufaransa.
 
Rais Dk. Mwinyi alisema kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar iko tayari kushirikiana na Wafanyabiashara wa Ufaransa na Taasisi mbali mbali za Ufaransa ili kuweza kuleta maendeleo kwa wananchi wa Unguja na Pemba.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Translate »