LEO Rais Samia Suluhu Hassan amechoma chanjo ya COVID 19.

LEO Rais Samia Suluhu Hassan amechoma chanjo ya COVID 19.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Samia Suluhu Hassan leo Julai 28,2021 amepata chanjo ya Covid- -19 mbele ya viongozi mbalimbali wa dini na Serikali ikulu jijini Dar es salaam. Rais Samia amepata chanjo hilo leo ikiwa ni siku ya ufunguzi wa utoaji chanjo hapa nchi na kuwatoa hofu watanzania kuwa chanjo hiyo

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Samia Suluhu Hassan akipata chanjo ya Covid-19 Ikulu jijini Dar es Salaam leo Julai 28, 2021
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Kassim Majaliwa akipata chanjo ya Covid-19 Ikulu jijini Dar es Salaam leo Julai 28, 2021
Jaji Mkuu wa Tanzania, Profesa Ibrahim Juma  akipata chanjo ya Covid-19 Ikulu jijini Dar es Salaam leo Julai 28, 2021
Mkuu wa Majeshi  Tanzania (CDF) Venance Mabeyo, akipata chanjo ya Covid-19 Ikulu jijini Dar es Salaam leo Julai 28, 2021
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Amos Makalla akipata chanjo ya Covid-19 Ikulu jijini Dar es Salaam leo Julai 28, 2021

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Samia Suluhu Hassan leo Julai 28,2021 amepata chanjo ya Covid- -19 mbele ya viongozi mbalimbali wa dini na Serikali ikulu jijini Dar es salaam.

Rais Samia amepata chanjo hilo leo ikiwa ni siku ya ufunguzi wa utoaji chanjo hapa nchi na kuwatoa hofu watanzania kuwa chanjo hiyo ni salama na hivyo itatolewa kwa wote watakao hitaji kuchajwa.

Mbali na rais Samia, Viongozi wengine waliochanjwa leo ni pamoja na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Kassim Majaliwa na mkwe Mama Mery Majaliwa,Waziri wa Afya Dkt.Dorothy Gwajima, Jaji Mkuu wa Tanzania, Wakuu wa vyombo vya Ulinzi na Usalama, ViongoZI wa Dini na Serikali.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan leo tarehe 28 Julai, 2021 amezindua utolewaji wa chanjo ya UVIKO 19 na kuongoza Watanzania kupata chanjo hiyo katika viwanja vya Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Akizungumza kabla ya kuanza zoezi hilo, Mhe. Rais Samia amewatoa hofu Watanzania kuwa chanjo hiyo ni salama na yeye kama Rais na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama asingejitoa mwenyewe kujipeleka kwenye hatari huku akijua kuwa ana majukumu makubwa yanayomtegemea.

“ Nimekubali kwa hiyari yangu kuchanja nikijua ndani ya mwili wangu nina chanjo kadhaa ambazo nimeishi nazo kwa miaka 61 sasa, tangu tumezaliwa tumepata chanjo zisizopungua tano na hii ya sita na nyingine nilizochanja nikiwa nasafiri, hivyo sioni hatari ya chanjo hii baada ya wanasayansi kujiridhisha na zimekuja nchini na wanasayansi wetu nchini wamejiridhisha mimi niko tayari kuchanja” amesema Mhe. Rais Samia.

Mhe. Rais Samia amewaomba Watanzania kwa hiyari yao kushiriki katika zoezi hilo la  chanjo  hiyo ya UVIKO 19 ila waendelee kujihadhari na ugonjwa huo.

Aidha, Mhe. Rais Samia amesema kama hujaguswa na maradhi hayo ya UVIKO 19 au watu wako wa karibu unaweza kubeza chanjo ila walioguswa wanatamani kupata chanjo hiyo kwa haraka iwezekanavyo.

Amesema amekuwa akipokea jumbe mbalimbali za simu kutoka kwa baadhi ya Watanzania wakimuuliza jinsi ya kupata chanjo hizo ambapo amesema kwa sasa Serikali inaendelea kuratibu upatikanaji wa chanjo za kutosha ili kuwezesha wananchi wengi kupata chanjo hizo.

Kwa upande wake Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia , Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima amewataka wananchi kuwapuuza wale wote wanaopotosha kuhusu chanjo hizo za UVIKO 19 na kusisitiza kuwa ni salama kwa afya baada ya  wataalam wetu nchini  kujiridhisha kabla ya kuamua kufanyika kwa zoezi hilo.

Mhe. Dkt. Gwajima amewaomba viongozi wa dini, siasa na viongozi wengine katika makundi mbalimbali na Watanzania kwa ujumla kupokea chanjo hiyo kwa kuwa ni silaha ya kisasa katika kukabiliana na UVIKO 19.

Mhe. Waziri Dkt. Gwajima amebainisha kuwa nchi ambazo zimefanya zoezi kama hili la  uchanjaji zimepata matokeo mazuri ikiwemo kupunguza maambukizi, kupunguza idadi ya wagonjwa wanaohitaji kulazwa pamoja na  kupunguza vifo vitokanavyo na UVIKO 19.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »