Wanafunzi watatu wafariki dunia kwa kufunikwa na kifusi wilayani Mpwapwa

Wanafunzi watatu wafariki dunia kwa kufunikwa na kifusi wilayani Mpwapwa

Na Barnabas Kisengi, Mpwapwa Waziri wa Ofisi ya Rais tawala za mikoa na serikali za mitaa (Tamisemi) Ummy Mwalimu ameitaka kamati ya Ulinzi na usalama ya mkoa akishirikiana na kamati ya Ulinzi ya wilaya ya Mpwapwa kuchunguza tukio la WANAFUNZI watatu wa shule ya msingi mbori wilayani Mpwapwa waliofariki dunia  kufuatia ajali ya kufukiwa na

Na Barnabas Kisengi, Mpwapwa


Waziri wa Ofisi ya Rais tawala za mikoa na serikali za mitaa (Tamisemi) Ummy Mwalimu ameitaka kamati ya Ulinzi na usalama ya mkoa akishirikiana na kamati ya Ulinzi ya wilaya ya Mpwapwa kuchunguza tukio la WANAFUNZI watatu wa shule ya msingi mbori wilayani Mpwapwa waliofariki dunia  kufuatia ajali ya kufukiwa na kifusi wakati wakichimba mchanga waliotumwa na walimu wao  kwa ajili ya ujenzi wa kujengea matundu ya vyoo vya shule.

        Kauli hiyo ameitoa waziri  ummi mwalimu alipo  hudhuria ibada ya mazishi ya wanafunzi hao walio fariki kwa kuangukiwa na kifusi katika   wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma. 


Ummy amesema pamoja na kuziagiza kamati hizo za Ulinzi na usalama pia ameagiza uongozi wa Idara ya elimu wilaya kuwahamisha walimu Wote shuleni hapo na kupelekwa walimu  wengine shuleni hapo
 ” nasema licha ya kuwahamisha walimu hawa pia watachunguza tukio zima na  kubaini Kama kuna uzembe Umetokea basi Wahusika  watachukuliwa hatua za kinidhamu na kisheria kama miongozo ya idara ya elimu inavyo onyesha kwakuwa tukio limetokea basi wananchi muwe watulivu kwakuwa serikali yenu iko makini na tutawajulisha baada ya uchunguzi kukamilika”amesema waziri ummy.


Mwenyekiti wa kamti ya ulinzi na usalama ambae pia ni mkuu wa wilaya ya Mpwapwa Japhet Maganga amethibitisha kutokea kwa tukio hilo lililosababishwa na kufusi cha mcahanga kuwaangua wanafunzi hao na kufariki dunia


Alisema tukio hilo lilitokea majira ya saa tatu na nusu asubuhi katika korongo la manamba ambapo walimu waliwaagiza wanafunzi hao kwenda kuchukua mchanga korongoni.


Maganga amewataja watoto waliofariki katika tukio hilo ni  Rehema Alex ,Daud Machea na  Ezra  Lukas   na wengine walio jeruhiwa  ni Arapha Athuman  ,Nelly  Daudi, Yunis  Musa na Mwijuma Michael ambao wanaendelea na matibabu katika hospitali benjamini mkapa wilaya Mpwapwa walipo lazwa na hali zao zinaendelea vizuri hadi sasa.


Aidha Maganga amesema kufuatia tukio hilo serikali  imegharamia gharama zote za mazishi ya wanafunzi hao wote watatu waliofariki dunia katika tukio hilo
Hata hivyo mkuu wa wilaya huyo amepiga marufuku shughuli zote za  kubeba  za kimaendeleo kufanywa na wanafunzi bali amewataka wazazi ndio wafanye shughuli hizo  kwa mujibu wa vikao vyao serikali za vijiji na wanafunzi wasihusishwe katika shughuli za ujenzi wowote mashuleni.


Kwa uapnde wake  Tabibu Mfawidhi wa  Zahati ya mbori Elizabeth Sendeu amekili kupokea miili mitatu ya wanafunzi waliofariki dunia na majerhi sita ambao amesema mmoja alipatiwa huduma ya kwanza na kurudi na nyumbani na wengine walipekwa hospitali ya wilaya kwa matibabu zaidi.


Mmoja wa wakazi wa kijiji hicho Daud Ngumi amesema  lazima walimu wanapo watuma watoto kwenye kazi za maendeleo ya shule wawe na usimamizi wa walimu au viranja wao wenye umri mkubwa.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Translate »