Na Barnabas Kisengi, Kwimba Mwanza. Jitihada za Serikali kupitia wizara ya Elimu na Mafunzo ya ufundi za ukarabati wa Miundombinu vyuo vya maendeleo ya wananchi nchini [FDC]umechochea ongezeko la udahili wa wanafunzi katika chuo cha Maendeleo ya Wananchi Malya FDC kutoka wanafunzi 60 hadi zaidi ya wanafunzi 500 kwa mwaka. Hayo yamebainishwa leo Julai 29,2021 jijini Mwanza na Mratibu

Na Barnabas Kisengi, Kwimba Mwanza.
Jitihada za Serikali kupitia wizara ya Elimu na Mafunzo ya ufundi za ukarabati wa Miundombinu vyuo vya maendeleo ya wananchi nchini [FDC]umechochea ongezeko la udahili wa wanafunzi katika chuo cha Maendeleo ya Wananchi Malya FDC kutoka wanafunzi 60 hadi zaidi ya wanafunzi 500 kwa mwaka.
Hayo yamebainishwa leo Julai 29,2021 jijini Mwanza na Mratibu wa mafunzo chuo cha Maendeleo ya Wananchi Malya-FDC George Lubinza wakati akifanya mahojiano na Morning Star Radio ambapo amesema mwaka 2015 udahili ulikuwa chini lakini sasa upo hadi asilimia 80%.
Aidha,Lubinza amesema chuo hicho kimeanzisha program ya elimu haina mwisho kinachomwezesha mwanafunzi wa kike aliyekatishwa masomo kutokana na mimba kuendelea na masomo na hadi sasa kukiwa na wanafunzi wa kike 97 huku pia kukianzishwa program ya Malezi[ECD] .
Domina Damat ni miongoni mwa wanafunzi wanaosomea kozi ya malezi ameleezea jinsi jamii ilivyo na mtazamo hasi juu ya kozi hiyo ya malezi ya watoto.
Chuo cha Maendeo ya Wananchi Malya FDC ni miogoni mwa Vyuo 54 nchini vilivyoanzishwa mwaka 1975 chini ya Muasisi ya Taifa la Tanzania Mwalimu Julius Kambarage Nyerere lakini kwa muda mrefu vilitelekezwa na kwa utambua umuhimu wa vyuo hivi katika jamii Serikali imeamua kuviboresha kwa kukarabati miundombinu pamoja na kuoneza kozi.
Leave a Comment
Your email address will not be published. Required fields are marked with *