USAJILI WA WAKULIMA WASHIKA KASI

USAJILI WA WAKULIMA WASHIKA KASI

Na Mwandishi Wetu-Dodoma Wizara ya Kilimo kwa kushirikiana na wizara ya Ofisi ya Rais TAMISEMI, Sekretarieti za Mikoa na Halmashauri za Serikali za Mitaa zinaendelea na usajili wa wakulima kwenye mfumo wa M-Kilimo ili waweze kutambuliwa, kutoa huduma kwa njia ya simu na pia Serikali kutoa huduma zingine kwa urahisi. Mpaka sasa hivi zaidi ya

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Prof. Siza Tumbo

Na Mwandishi Wetu-Dodoma

Wizara ya Kilimo kwa kushirikiana na wizara ya Ofisi ya Rais TAMISEMI, Sekretarieti za Mikoa na Halmashauri za Serikali za Mitaa zinaendelea na usajili wa wakulima kwenye mfumo wa M-Kilimo ili waweze kutambuliwa, kutoa huduma kwa njia ya simu na pia Serikali kutoa huduma zingine kwa urahisi.

Mpaka sasa hivi zaidi ya nusu ya mikoa yote Tanzania Bara, Mikoa 14 imeweza kusajili na kufikia asilimia 50 au zaidi kwenye mfumo huo wa M-Kilimo.

Akizungumzia hali ya usajili wa wakulima mpaka hivi sasa, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Prof. Siza Tumbo amesema kuwa Mikoa 12 bado ipo chini ya asilimia 50 kwenye usajili wa wakulima.

Prof. Tumbo ameeleza kuwa Mikoa minne (4) ambayo ni Njombe, Arusha, Simiyu na Singida imeweza kufikia lengo la asilimia 100 na zaidi. Wizara ya Kilimo inaipongeza sana mikoa hii kwa kufikia hatua hiyo.

Amesema kuwa Mikoa ya Shinyanga, Kagera na Dar-es-Salaam bado wapo chini ya asilimia 30, hivyo kuwasihi kuongeza kasi ili kufikia malengo ya Serikali.

Pia, Wizara ya Kilimo inatoa shukrani za dhati kwa Wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya, Watendaji Wakuu na Wakati kayika ngazi ya Mikoa na Wilaya/Halmashauri na Maafisa Kilimo na Wagani wote kwa kazi kubwa ya kuwezesha, kuhamasisha na kusajili wakulima kwenye mfumo wa M-Kilimo

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »