Shule za msingi 38 zimefutiwa matokeo ya darasa la saba baada ya kufanya udanganyifu.

Shule za msingi 38 zimefutiwa matokeo ya darasa la saba baada ya kufanya udanganyifu.

Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA), limefuta matokeo ya mitihani ya Taifa ya darasa la 7 kwa shule 38, ambazo zimebainika kufanya udanganyifu kwenye mitihani hiyo iliyofanyika Oktoba 7 na 8, 2020, na kuwafutia matokeo watahiniwa 1,059, baada ya kubainika wamefanya udanganyifu. Taarifa hiyo imetolewa hii leo Novemba 21, 2020, na Katibu Mtendaji wa Baraza hilo

KATIBU MTENDAJI WA NECTA DKT.CHARLES MSONDE.

Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA), limefuta matokeo ya mitihani ya Taifa ya darasa la 7 kwa shule 38, ambazo zimebainika kufanya udanganyifu kwenye mitihani hiyo iliyofanyika Oktoba 7 na 8, 2020, na kuwafutia matokeo watahiniwa 1,059, baada ya kubainika wamefanya udanganyifu.

Taarifa hiyo imetolewa hii leo Novemba 21, 2020, na Katibu Mtendaji wa Baraza hilo Dkt. Charles Msonde, ambapo amesema kuwa mbali na hao Baraza hilo pia, limezuia matokeo ya watahiniwa 110 ambao waliugua wakati wa kufanya mitihani hiyo na hivyo watalazimiika kurudia mtihani mwakani kwa mujibu wa sheria.

Shule zilizofutiwa matokeo ni Mafiri, Kibogoji, Ng’wambe, Digalama, Dihinda za Halmashauri ya Mvomero,shule za msingi za Nyawa A Halmashauri ya Bariadi vijijini, Ngiloli, Nguyami, Ibuti, Ihenje, Bwawani, Mogohigwa, Chakwale na Msingisi za Halmashauri ya Gairo.

Dkt.Msonde amesema shule nyingini zilizofungiwa ni Sikonge , Chabutwa, Usagari, Uyui za mkoani Tabora, Siashimbwe iliyopo Moshi Kilimanjaro, Dominion ya mkoani Arusha, Matogoro ya Tandahimba Mtwara, Ng’arita ya Bariadi vijijini mkoani Simiyu, Olkitikiti Kiteto iliyopo Manyara na Nyamimina Buchosa ya mkoani Mwanza.

Aidha katika hatua nyingine Dkt. Msonde, amesema ufaulu wa wanafunzi wa darasa la saba, umeongezeka kwa wanafunzi kupata alama hadi 250 kwa masomo yote na hivyo kufikia asilimia 82.68

Kuhusu mitihani ya kidato cha nne inayotarajiwa kuanza wiki ijayo, Dkt Msonde amewahimiza walimu na wanafunzi kuacha kushiriki vitendo vyovote vya udanganyifu kwa kuwa wakibainika watafutiwa matokeo yao ya mitihani

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »