CHANJO CORONA LAZIMA WANAOTAKA KWENDA KUISHI SAYARI YA MARS

CHANJO CORONA LAZIMA WANAOTAKA KWENDA KUISHI SAYARI YA MARS

Shirika la anga na unajimu la nchini Marekani NASA limetoa vigezo kwa watu watakaochukuliwa ili kwenda kuanzisha maisha mapya katika sayari jirani ya Mars. Shirika hilo limesema mpango wa kuhamisha makazi ya binadamu kwenda kuishi kwenye sayari hiyo jirani unatazamiwa kuanza mwaka 2037. Sayari hiyo inayojulikana kama sayari nyekundu yaani Red Planet kutokana na muonekano wake wa

Shirika la anga na unajimu la nchini Marekani NASA limetoa vigezo kwa watu watakaochukuliwa ili kwenda kuanzisha maisha mapya katika sayari jirani ya Mars.

Shirika hilo limesema mpango wa kuhamisha makazi ya binadamu kwenda kuishi kwenye sayari hiyo jirani unatazamiwa kuanza mwaka 2037.

Sayari hiyo inayojulikana kama sayari nyekundu yaani Red Planet kutokana na muonekano wake wa rangi nyekundu inapotazamwa kupitia hadubini ndiyo sayari inayoleta matumaini ya uwezekano wa maisha ukilinganisha na sayari nyingine katika mfumo wa jua.

Tayari vyombo mbalimbali vya anga vimeshatumwa katika sayari hiyo ili kuangalia uwezekano wa wanadamu kuishi katika sayari hiyo na chombo cha mwisho kilirushwa mnamo mwezi wa pili mwaka huu.

Shirika hilo limesema watu wanaokidhi vigezo vya kwenda kuanzisha maisha mapya katika sayari ya Mars ni wale tu waliopokea chanjo, wawe na umri wa kuanzia miaka 30-55 na wawe wamehitimu shahada ya uzamili yaani Masters katika masomo ya uhandishi, teknolojia, sayansi na hisabati.

Mpango huo wa mchujo wa watu wataokidhi vigezo utaanza mwakani ambapo utafanyika jijini Texas nchini Marekani

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »