KAMATI YA KUDUMA YA BUNGE YA KILIMO, MIFUGO NA MAJI YAPONGEZA UWEKEZAJI WA MAZAO YA MBOGAMBOGA, MATUNDA NA MAZAO YA MIZIZI

KAMATI YA KUDUMA YA BUNGE YA KILIMO, MIFUGO NA MAJI YAPONGEZA UWEKEZAJI WA MAZAO YA MBOGAMBOGA, MATUNDA NA MAZAO YA MIZIZI

Na Mwandishi wetu-Kilimanjaro Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji Mhe Dkt. Christine Ishengoma ameipongeza Wizara ya Kilimo pamoja na Taasisi Kilele inayojihusisha na ulimaji wa mbogamboga, maua na mazao ya bustani TAHA kwa uwekezaji mzuri nchini. Dkt Ishengoma ametoa pongezi hizo tarehe 14 Agosti 2021 mara baada ya kutembelea

Waziri wa Kilimo Mhe Prof. Adolf Mkenda akisisitiza jambo wakati akizungumza na Mtendaji Mkuu wa TAHA Dkt Jacqueline Mkindi walipotembelea shamba la kampuni ya uzalishaji wa ndizi pamoja na karanga aina ya Macademia ya Macjaro Ltd iliyopo eneo la Machame katika Wilaya ya Hai Mkoa wa Kilimanjaro wakati wa ziara ya kikazi ya kamati ya kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji. Tarehe 14 Agosti 2021
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni inayohusika na uzalishaji wa vikonyo vya maua  ya Vasso Agroventures ltd Ndg Fons Nijenhuis akitoa ufafanuzi kuhusu uzalishaji wa maua mbele ya wajumbe wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji wakati wa ziara ya kikazi katika shamba hilo lililopo Kijiji cha Mkoringa kilichopo Kata ya Kibosho Wilaya ya Moshi Vijijini Mkoani Kilimanjaro. Tarehe 14 Agosti 2021.
Waziri wa Kilimo Mhe Prof. Adolf Mkenda akimsikiliza kwa makini Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni inayohusika na uzalishaji wa vikonyo vya maua  ya Vasso Agroventures ltd Ndg Fons Nijenhuis akitoa ufafanuzi kuhusu uzalishaji wa maua mbele ya wajumbe wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji wakati wa ziara ya kikazi katika shamba hilo lililopo Kijiji cha Mkoringa kilichopo Kata ya Kibosho Wilaya ya Moshi Vijijini Mkoani Kilimanjaro. Tarehe 14 Agosti 2021.
Waziri wa Kilimo Mhe Prof. Adolf Mkenda akishiriki palizi kwenye migomba alipotembelea shamba la kampuni ya uzalishaji wa ndizi pamoja na karanga aina ya Macademia ya Macjaro Ltd iliyopo eneo la Machame katika Wilaya ya Hai Mkoa wa Kilimanjaro wakati wa ziara ya kikazi ya kamati ya kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji. Tarehe 14 Agosti 2021.
Waziri wa Kilimo Mhe Prof. Adolf Mkenda akisisitiza jambo wakati akizungumza na Mtendaji Mkuu wa TAHA Dkt Jacqueline Mkindi (Kushoto) na Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji Mhe Almas Maige (Kulia) walipotembelea shamba la kampuni ya uzalishaji wa ndizi pamoja na karanga aina ya Macademia ya Macjaro Ltd iliyopo eneo la Machame katika Wilaya ya Hai Mkoa wa Kilimanjaro wakati wa ziara ya kikazi ya kamati ya kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji. Tarehe 14 Agosti 2021
Waziri wa Kilimo Mhe Prof. Adolf Mkenda akizungumza na Meneja Ubora wa Kampuni inayohusika na uzalishaji, ununuzi na usafirishaji wa maharage Machanga ya African Vegetable Limited liyopo eneo la Machame katika Wilaya ya Hai Mkoa wa Kilimanjaro wakati wa ziara ya kikazi ya kamati ya kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji. Tarehe 14

Na Mwandishi wetu-Kilimanjaro

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji Mhe Dkt. Christine Ishengoma ameipongeza Wizara ya Kilimo pamoja na Taasisi Kilele inayojihusisha na ulimaji wa mbogamboga, maua na mazao ya bustani TAHA kwa uwekezaji mzuri nchini.

Dkt Ishengoma ametoa pongezi hizo tarehe 14 Agosti 2021 mara baada ya kutembelea na kukagua shamba la kampuni ya African Vegetable Limited, Shamba la Macjaro Limited lililopo Machame Wilayani Hai na Shamba la Vasso Agroventures Ltd lililopo katika kijiji cha Mkoringa kata ya Kibosho Wilaya ya Moshi Vijijini.

Mhe Ishengoma ameahidi kuzisimamia na kuhakikisha kuwa changamoto mbalimbali zinazoikabili sekta hiyo nchini zinatatuliwa na serikali kupitia Wizara ya kilimo ili kuongeza uwekezaji na ajira kwa watanzania wengi.

Akizungumza katika ziara hiyo Waziri wa Kilimo Mhe Prof. Adolf Mkenda amesema kuwa sekta ya mbogamboga, maua na mazao ya bustani haina changamoto ya soko hivyo wananchi wanapaswa kuuona umuhimu wa kuwekeza katika sekta hiyo.

Amesema kuwa sehemu kubwa ya mazao mengi nchini wakulima hulima bila kujua soko lilipo lakini katika sekta hiyo mkulima anaweza kulima huku akiwa na uhakika wa soko la ndani nan je ya nchi.

Amesema kuwa serikali inatambua umuhimu wa zao la ndizi hivyo tayari imejipanga kufanya mkutano maalumu kwa ajili ya kuweka mikakati ya kilimo cha zao hilo ikiwa ni pamoja na kufungua maabara ya utafiti ili kuongeza uzalishaji wa mazao.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi Kilele inayojihusisha na ulimaji wa mbogamboga, maua na mazao ya bustani-TAHA Dkt Jacqueline Mkindi amesema kuwa sekta hiyo imeendelea kupata ushirikiano madhubuti kutoka serikalini jambo ambalo linaimarisha uhusiano wa kiutendaji.

Amesema kuwa ziara hiyo ya kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji imetoa fursa ya kuimarisha sekta hiyo ikiwa ni pamoja na kuongeza uwekezaji utakaotoa fursa kubwa ya ajira kwa vijana ikiwa ni pamoja na kuimarisha kipato cha wananchi.

Amesema Tanzania ina ardhi yenye rutuba nzuri, uwepo wa maji ya kutosha hivyo matarajio yake ni kujipanga vizuri kwenye mifumo na miundombinu ya kufikia masoko ili kutengeneza mapato kwa mwaka kwa zaidi ya Dola za Kimarekani Bilioni 6.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »