“HAKUNA MFANYABIASHARA ATAKAEPEWA KIBALI KUAGIZA SUKARI KAMA SIO MZALISHAJI” WAZIRI MKENDA.

“HAKUNA MFANYABIASHARA ATAKAEPEWA KIBALI KUAGIZA SUKARI KAMA SIO MZALISHAJI” WAZIRI MKENDA.

Serikali imesema kuwa itasimamia sheria na taratibu iliyojiwekea kwenye usimamizi wa mazao mbalimbali ikiwemo miwa, hivyo haitatoa kibali kwa wafanyabiashara wa sukari badala yake kibali kitatolewa kwa wazalishaji wa ndani kama kutakuwa na uhitaji. Imebainisha kuwa kwa sasa nchini kuna ziada ya Tani Zaidi ya 70,000 za sukari hivyo serikali haiwezi kutoa kibali chochote cha

Waziri wa Kilimo Mhe Prof. Adolf Mkenda (Katikati) akisisitiza jambo wakati wa mkutano na wazalishaji wakubwa wa sukari nchini uliofanyika katika ukumbi wa Wizara ya Kilimo Maarufu “Kilimo IV” Jijini Dodoma, tarehe 16 Agosti 2021.Wengine pichani ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Ndg Andrew Massawe (Kulia) na Mwenyekiti wa Wazalishaji wakubwa wa sukari Tanzania Ndg Seif Ally Seif (Kushoto).

Waziri wa Kilimo Mhe Prof. Adolf Mkenda (Kushoto) pamoja na Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Ndg Andrew Massawe wakifuatilia kwa makini mkutano wa wazalishaji wakubwa wa sukari nchini uliofanyika katika ukumbi wa Wizara ya Kilimo Maarufu “Kilimo IV” Jijini Dodoma, tarehe 16 Agosti 2021

Mwenyekiti wa wazalishaji wakubwa wa sukari nchini (Kushoto) Ndg Seif Ally Seif akichangia mada wakati wa mkutano na Waziri wa Kilimo Mhe Prof. Adolf Mkenda wakati wa mkutano wa wazalishaji wakubwa wa sukari nchini uliofanyika katika ukumbi wa Wizara ya Kilimo Maarufu “Kilimo IV” Jijini Dodoma, tarehe 16 Agosti 2021.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Ndg Andrew Massawe akisisitiza jambo wakati wa mkutano wa wazalishaji wakubwa wa sukari nchini uliofanyika katika ukumbi wa Wizara ya Kilimo Maarufu “Kilimo IV” Jijini Dodoma, tarehe 16 Agosti 2021



Serikali imesema kuwa itasimamia sheria na taratibu iliyojiwekea kwenye usimamizi wa mazao mbalimbali ikiwemo miwa, hivyo haitatoa kibali kwa wafanyabiashara wa sukari badala yake kibali kitatolewa kwa wazalishaji wa ndani kama kutakuwa na uhitaji.


Imebainisha kuwa kwa sasa nchini kuna ziada ya Tani Zaidi ya 70,000 za sukari hivyo serikali haiwezi kutoa kibali chochote cha uagizaji wa sukari nje ya nchi wakati uzalishaji unaendelea nchini.


Waziri wa Kilimo Mhe Prof. Adolf Mkenda ametoa kauli hiyo ya serikali leo tarehe 16 Agosti 2021 mara baada ya kumalizika kwa kikao cha kazi na wazalishaji wakubwa wa sukari hapa nchini kilichofanyika katika ukumbi wa Wizara ya Kilimo Maarufu “Kilimo IV” Jijini Dodoma.


Amesema kuwa serikali kuendelea kutoa kibali kuagiza sukari nje ya nchi sio sahihi kwani inahatarisha uzalishaji wa sukari nchini jambo linalowakosesha ajira watanzania wengi huku likiwakosesha soko la miwa kwa wakulima ambao miwa yao huchomwa kutokana na uwezo mdogo wa viwanda vya ndani.


“Ninawaomba sana wafanyabiashara wote nchini watambue kuwa serikali inapenda sana wapate faida kwenye biashara zao lakini hii ya sukari waache tupambane ili tuweze kuzalisha ndani ya nchi” Amekaririwa Waziri Mkenda
Kauli hiyo ya Waziri wa Kilimo inajili wakati ambapo imebainika kuwa kumekuwa na barua nyingi zinazowasilishwa Bodi ya Sukari kwa ajili ya maombi ya kibali cha kuagiza sukari nje ya nchi.


“Mimi ndio msimamizi wa sheria kwahiyo msimuhangaishe sana Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Sukari Tanzania kwamba yeye anakataa kuwapa ruhusa ya kuingiza sukari, sheria haimruhusu na wala hainiruhusu mimi kutoa kibali hicho” Mhe Mkenda alisema.


Sheria hiyo imeilekeza Wizara ya Kilimo kuhakikisha kuwa sukari iingizwe kwa utaratibu ili kuwekeza Zaidi nchini, hivyo sheria hiyo haitabadilishwa kama watu wanavyofikiri.


Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama cha wazalishaji wa sukari Tanzania (TSPA) Ndg Seif Ally Seif amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kusimamia uimarishaji wa viwanda nchini.


Amesema kuwa Uwekezaji wa sukari ni wa muda mrefu hivyo serikali imeendelea kutoa hamasa kwa wawekezaji wa ndani na wa nje katika uwekezaji wa viwanda mbalimbali ikiwemo vya sukari

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Translate »